VODACOM YAUNGA JUHUDI ZA SERIKALI KUHAMIA DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 10 May 2019

VODACOM YAUNGA JUHUDI ZA SERIKALI KUHAMIA DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge, akikata utepe kuzindua ofisi mpya za kanda ya kati na duka la kisasa la Vodacom Tanzania Plc jijini Dodoma. Kampuni hiyo imezindua makao yake makuu ya Kanda ya Kati ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamishia shughuli zake Mji Mkuu kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu. Wa pili kulia ni Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde na Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Kati wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bi Grace Chambua. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Linda Riwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge akizungumza katika uzinduzi wa ofisi mpya za Kanda ya kati na duka la kisasa la Vodacom Tanzania Plc jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu ya mtandao huo.

Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa ofisi mpya na duka la kisasa la Vodacom Tanzania jana jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu.

Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa akizungumza katika uzinduzi wa ofisi mpya na duka la kisasa la Vodacom Tanzania jana jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu.

Mkuu wa Mauzo wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania, Bi Grace Chambua akizungumza katika uzinduzi wa ofisi mpya na duka la kisasa la Vodacom Tanzania jana jijini Dodoma. Kampuni hiyo imeunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake mji mkuu kwa kuhakikisha wanapata mawasiliano imara na huduma sanifu. Walio keti ni Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde (wa kwanza kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge (kati) na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania, Linda Riwa.

No comments:

Post a Comment