TIRA YAZINDUA KANUNI ZA BIMA KUPITIA BENKI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 20 May 2019

TIRA YAZINDUA KANUNI ZA BIMA KUPITIA BENKI

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Yamungu Kayandabila (mwenye tai nyeusi katikati) akizindua rasmi Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) pamoja naye ni viongozi mbalimbali wa taasisi za fedha na benki nchini walioshiriki uzinduzi huo.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Yamungu Kayandabila (mwenye tai nyeusi katikati) akizindua rasmi Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) pamoja naye ni viongozi mbalimbali wa taasisi za fedha na benki nchini walioshiriki uzinduzi huo.

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa taasisi za fedha na benki nchini wakiwa wameshika nakala za Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations) mara baada ya kuzinduliwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Yamungu Kayandabila juzi.

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk. Baghayo Saqware akizungumza na wanahabari mara baada ya uzinduzi wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations).

Mkurugenzi wa Leseni na Usimamizi wa Biashara, Samwel Mwiru kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) akitoa mada kwa washiriki kufafanua kanuni hizo kabla ya kuzinduliwa rasmi

Sehemu ya wageni waalikwa kutoka taasisi za fedha na mabenki nchini walioshiriki uzinduzi huo wakifuatilia mada.

Na Joachim Mushi

MAMLAKA ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimezindua Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations).

Akizindua rasmi kanuni hizo Jijini Dar es Salaam, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Yamungu Kayandabila amezitaka taasisi za fedha na benki nchini kuzizingatia katika utoaji wa huduma zao ili kuongeza ufanisi wa shughuli zao. Alisema kanuni hizo zitasaidia kusambaza huduma ya bima nchini kwani watu wengi bado hawajafikiwa.

“Ujio wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki nchini Tanzania umechelewa kidogo hivyo wadau wana kila sababu ya kuzingatia kwa manufaa ya pande zote watoa huduma na wanufaika,” alisema

Alisema endapo wadau watazizingatia kanuni hizo mapato katika sekta hiyo kiujumla yataongezeka kwa taifa, watoa huduma na watu wengi zaidi watafikiwa na huduma za bima. 

Aidha kwa upande wake, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk. Baghayo Saqware akizungumza katika hafla hiyo alisema licha ya manufaa lukuki ya uzinduzi wa kanuni hizo pia unalenga kueneleza ajenda ya TIRA ya kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma za bima nchini yaani bima kwa wote.

"Tunahitaji kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za Bima (access) nchini kwa kuongeza aina mbalimbali za bima kwa mahitaji mbalimbali, mfano mbadala wa uuzaji na usambazaji wa huduma za bima ikiwemo kutumia benki,” alisema

Kamishna huyo aliongeza kuwa inahitajika teknolojia rahisi na rafiki kwa ajili ya kusambaza bima, kununua bima, kuuza bima, kulipa mafao/madai ya bima, kusikiliza maoni na mahitaji ya wananchi, kuchakata na kuandikisha maombi ya bima," alisema Dk. Saqware.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa kanuni hizo ni muhimu katika kuendeleza sekta ya kifedha nchini na kusisitiza kuwa pato la taifa, hasa ukizingatia faida nyingi ambazo zitapatikana kwa benki zenyewe na watumiaji wa huduma za bima.

 Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali serikalini, makampuni ya bima, taasisi za kifedha, mawakala mbalimbali na wadau wa sekta ya bima na kudhaminiwa na BoT, Reliance Insurance, Heritage Insurance, Zanzibar Insurance, Chama Cha Watoa Huduma za Bima (ATI), NMB, CRDB Insurance, Metropolitan Life Tanzania, Jubilee Insurance, FSDT, Stanbic Bank, Smart Policy, Alliance Insurance, TPB Bank na Shirika la Bima la Taifa (NIC).


Mshereheshaji katika hafla ya uzinduzi wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations), Baby Kabae akitoa maelekezo anuai kabla ya uzinduzi huo.

Burudani kutoka kwa Mjomba Band chini ya Mrisho Mpoto akiendelea katika hafla ya uzinduzi wa Kanuni za Kutoa Huduma za Bima Kupitia Benki (Bancassurance regulations).

No comments:

Post a Comment