IKUPA ATOA MSAADA WA BAISKELI KWA MTOTO WENYE ULEMAVU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 16 May 2019

IKUPA ATOA MSAADA WA BAISKELI KWA MTOTO WENYE ULEMAVU

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akizungumza na mzazi wa mtoto huyo Bi. Magreth Leo alipokuwa akitoa msaada wa baiskeli.

Bi. Magreth Leo (katikati) akimwelezea jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (kushoto) kuhusu mtoto wake Happy Shabani Salumu wenye Ulemavu. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu Bi. Josephine Lyengi.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa akiwa na mtoto mwenye Ulemavu Happy Shabani Salumu mara baada ya kukabidi msaada wa baiskeli kwa mtoto huyo Mei 15, 2019 Jijini Dodoma.

Baadhi ya Maafisa wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu wakifuatilia maelezo ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipokuwa akitoa msaada wa baiskeli kwa mtoto Happy Shabani Salumu. Kushoto ni Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Joy Maongezi na Bi. Oliver Njogopa (katikati).

No comments:

Post a Comment