RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BAY KM 67 WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 8 April 2019

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BAY KM 67 WILAYANI MBINGA MKOANI RUVUMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Mbinga mjini mpaka Mbamba Bay km 67, sherehe zilizofanyika Mbinga mkoani Ruvuma. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Dkt. Alex Mubiru akishuhudia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Dkt. Alex Mubiru wa pili kutoka kushoto, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Godfrey Zambi (watatu kutoka kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Arch. Elius Mwakalinga (wapili kutoka kulia), Mwalikishi wa Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Chrisianus Ako (wa kwanza kulia) wakikata utepe kuzinduwa Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Mbinga mjini mpaka Mbamba Bay km 67.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi pamoja na Wanafunzi wa Shule mbalimbali za eneo la Kigonsera (hawaonekani pichani) Mbinga mkoani Ruvuma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa kwa wafuraha na wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Mbinga mjini kabla ya kuwahutubia.


No comments:

Post a Comment