Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa
(kushoto) akitoka katika moja ya majengo ya mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa
wa Magomeni Kota jijini Dar es Salaam alipofanya ziara yake leo.
|
Muonekano wa mtambo wa kisasa wa kuchanganya zege
katika mradi wa Ujenzi wa Nyumba za kisasa wa Magomeni Kota jijini Dar es
Salaam alipofanya ziara yake leo.
|
NAIBU
Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias John Kwandikwa ameagiza Wakala wa Majengo Nchini
(TBA) kuhakikisha wanamaliza Mradi wa Nyumba za Kisasa wa Magomeni Kota jijini
Dar es Salaam unamalizika kufikia mwezi Desemba mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Kwandikwa ametoa
msisitizo huo leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara kukagua maendeleo ya
mradi huo.
Amesema kuanzia sasa atakuwa akiutembelea mradi huo
kila mwezi ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa na hatimaye mradi ukamilike
Desemba kama ilivyoagizwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli alipoutembelea mradi
huo hivi karibuni.
"...Kuanzia leo nitahakikisha nawatembelea
hapa kama sio kila wiki basi kila mwezi, lengo langu ni kuhakikisha mradi huu
mkubwa unakamilika kwa wakati na wananchi hawa wapatao 656 waliokuwa wakiishi
hapa wanaingia na kuanza kuzitumia nyumba hizi," alisema Naibu Waziri.
Aidha aliongeza kuwa wizara yake itahakikisha
inafika eneo hilo kila mara kutatua changamoto zote ambazo zitakuwa zikihitaji
kutatuliwa na wizara hiyo, huku akionya itakuwa ni jambo la kushangaza endapo
mradi huo utasimama tena na kumlazimu Rais Dk. Magufuli arudi tena eneo hilo.
"...Sisi kama wizara tunataka endapo Mh. Rais
Dk. John Pombe Magufuli akija tena eneo la Magomeni Kota ni kufanya uzinduzi wa
nyumba zikiwa zimekamilika na si vinginevyo," alisisitiza Naibu Waziri
Kwandikwa akizungumza na viongozi na waandisi wa TBA wanaosimamia mradi huo.
Aliipongeza TBA kwa kitendo cha kuanza kutumia
mitambo ya kisasa ya kufyatua matofali, kuchanganya na kubeba zege hadi
gorofani jambo ambalo litaongeza kasi ya ujenzi na ufanisi katika mradi huo.
Aliwataka kuangalia namna ya kuanza haraka kufanya
kazi usiku na mchana kutokana na ujio wa mitambo hiyo. Alisema wazo la kuanza
kufanya kazi usiku na mchana licha ya kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi linatoa
fursa kwa vijana wengi sasa kuja kufanya kazi na kujipatia kipato.
Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Eng.
Jasper Lugemarila akizungumzia changamoto zilizokwamisha mradi huo awali,
alisema ilikuwa ni kupanda kwa bei ya zege ambayo walikuwa wakinunua pamoja na
bidhaa nyingine kama simenti, kokoto na nondo.
Alisema kwa sasa wamekwisha tatua changamoto hizo
baadha ya kuanza kutengeneza zege wenyewe kwa kutumia mitambo ya kisasa
inayoendeshwa na kompyuta.
"...Mwanzoni tulikuwa tunamimina zege kwa
kununua kutoka kwa wafanyabiashara hiyo, lakini walipoona mradi huu umeanza na
ni mkubwa wakatupandishia bei sana wakijua lazima twende kwao," alisema
Eng. Jasper Lugemarila.
Imetolewa
na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment