WAJUMBE WA BODI NA MENEJIMENTI YA BOHARI YA DAWA YA TAIFA UGANDA (NMS) WATEMBELEA MSD - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 12 March 2019

WAJUMBE WA BODI NA MENEJIMENTI YA BOHARI YA DAWA YA TAIFA UGANDA (NMS) WATEMBELEA MSD

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Fatma Mrisho (wa pili kulia), akiwaongoza wajumbe hao kwenda kuangalia Ghala la kuhifadhia dawa na vifaa tiba la MSD Keko jijini Dar es Salaam. 

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Fatma Mrisho (katikati) akimkabidhi zawadi  Meneja Mkuu wa NMS,  Bwana Moses Kamabare baada ya kutembelea MSD Dar es Salaam leo. Anayeshuhudia kushoto mwenye suti ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) Dkt. Fatma Mrisho, akizungumza na ujumbe huo.

Ujumbe huo ukiwa katika ghala la kuhifadhia dawa la MSD Keko jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

WAJUMBE wa Bodi na Menejimenti ya Bohari ya Dawa ya Taifa,nchini Uganda (NMS) wametembelea Bohari ya Dawa (MSD)  kubadilishana uzoefu na kujifunza namna MSD inavyoshirikiana na Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF).

Pamoja na mambo mengine Meneja Mkuu wa NMS Bwana Moses Kamabare ameipongeza MSD kwa kuboresha utendaji wake ikiwa ni pamoja na huduma zake kwa wateja na kufanya mabadiliko makubwa katika mnyororo wa ugavi.

Akizungumza na ugeni huo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Dkt. Fatma Mrisho amesema ushirikiano wa taasisi hizi mbili ni muhimu sana,hasa kwenye eneo la kubadilishana uzoefu kiutendaji, kwa nia ya kuboresha huduma.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amesema MSD imefanya maboresho makubwa kiutendaji,na ni siri kubwa ya mafanikio katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment