TUGHE MKOA WA TEMEKE WATOA MSAADA KWA YATIMA WA KITUO CHA HIARI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 15 March 2019

TUGHE MKOA WA TEMEKE WATOA MSAADA KWA YATIMA WA KITUO CHA HIARI

Wafanyakazi wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa Mkoa wa Temeke, wakiwa wamewabeba watoto Yatima wanaolelewa katika Kituo cha Hiari kilichopo Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam  walipokwenda kutoa msaada leo wa vyakula na vitu mbalimbali zikiwemo nguo ikiwa ni moja ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofikia tamati Machi 8, 2019.

Mratibu wa utoaji msaada huo ambaye pia ni  Katibu wa Tughe mkoa wa Temeke, Litson Magawa, akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo.

 Mratibu wa Jinsia wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Taifa, Nsubisi Mwasandende (kulia), akizungumza wakati wa kutoa msaada huo.

 Katibu wa Kamati ya Wanawake Tawi la Bohari ya Dawa (MSD) Theresia Mmbaga, akimkabidhi kiroba cha unga, Mama Mlezi wa Kituo hicho, Aminajati Kilemia wakati wa kukabidhi msaada huo.

  Katibu wa Kamati ya Wanawake Tawi la Bohari ya Dawa (MSD) Theresia Mmbaga, akimkabidhi fedha Mama mlezi wa kituo hicho.

 Katibu wa Kamati ya Wanawake Tawi la Bohari ya Dawa (MSD) Theresia Mmbaga, akimkabidhi dawa za meno kwa niaba ya wenzake mtoto Jamila Hiari.

 Mjumbe wa Tughe, Mkoa wa Dar es Salaam wa Kamati ya Wanawake kupitia Mkoa wa Temeke, Mawazo Lugusha (kulia), akizungumza wakati wa kutoa msaada huo.

 Mama Mlezi wa Kituo hicho, Aminajati Kilemia, akitoa neno na shukurani baada ya kupokea msaada huo.

Wawakilishi wa Wafanyakazi wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa Mkoa wa Temeke wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi msaada huo.

Na Dotto Mwaibale

WAFANYAKAZI wa Taasisi za Umma wametakiwa kujenga tabia ya kusaidia jamii zenye mahitaji mbalimbali badala ya kuiachia serikali kufanya hivyo.

Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Jinsia wa Chama cha Wafanyakazi (TUGHE) Taifa, Nsubisi Mwasandende wakati wafanyakazi wa Tughe mkoa wa Temeke wakipokuwa wakitoa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto Yatima wa Kituo cha Hiari kilichopo Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni moja ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo ilifikia tamati Machi 8, 2019.

"Wito wangu kwetu sisi wafanyakazi wa taasisi za umma tujenge utamaduni wa kusaidia jamii zenye changamoto mbalimbali badala ya kuiachia serikali kufanya hivyo" alisema Mwasandende.

Katibu wa Kamati ya Wanawake Tawi la Bohari ya Dawa (MSD) Theresia Mmbaga alisema ni muhimu kwa wafanyakazi wa taasisi za umma kuimarisha umoja wao na ushirikiano katika kusaidia jamii kama wao Tughe Mkoa wa Temeke walivyofanya.

Mjumbe wa Tughe, Mkoa wa Dar es Salaam wa Kamati ya Wanawake kupitia Mkoa wa Temeke, Mawazo Lugusha alisema sasa ni mwaka wa tatu wamekuwa wakisaidia jamii katika maeneo mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam na kuwa utaratibu huo wataendelea kuuhimarisha kila mwaka.

Katibu wa Tughe mkoa wa Temeke, Litson Magawa alisema huu ni mwanzo tu na kuwa wanajipanga kufanya makubwa miaka ijayo kwa ajili ya kusaidia jamii zenye changamoto.

Mlezi wa Kituo hicho cha Yatima Aminajati Kilemia alishukuru Tughe Mkoa wa Temeke kwa msaada huo na kuelezea kuwa umetoa faraja kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.

Alisema changamoto kubwa waliyonayo ni nyumba ya kuishi watoto hao ambapo alisema hiyo inayotumika sasa wamepanga na kila mwezi wanalipa sh.250,000 na kuwa haikidhi mahitaji kutokana na ongezeko la watoto kutoka maeneo mbalimbali baada ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia.

Alisema katika kituo hicho mahitaji halisi ni watoto 34 lakini idadi hiyo inapanda hadi kufika watoto 54. 

No comments:

Post a Comment