Katibu wa Itikadi na Uenezi
CCM Mkoa wa Iringa, Ramadhani Baraza akiongea na wanafunzi na wazazi wa Shule ya Sekondari ya Nyerere wakati wa mahafali ya kidato cha sita akimwakilisha mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Iringa (MNEC), Salim Asas aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi
CCM Mkoa wa Iringa, Ramadhani Baraza akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nyerere fedha zilizotolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Iringa (MNEC), Salim Asas kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba ya walimu wa shule hiyo.
NA
FREDY MGUNDA, IRINGA
MJUMBE
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Iringa (MNEC), Salim Asas
amechangia kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa
shule ya sekondari ya Nyerere iliyopo katika Kata ya migoli mkoani Iringa
Akimwakilisha
MNEC, Salim Asas wakati wa mahafali ya kidato cha sita katika shule
hiyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi
CCM Mkoa wa Iringa, Ramadhani Baraza alisema shule hiyo inakabiliwa na
upungufu wa nyumba za walimu na tayari ameona jitihada zinazoendelea hivyo
kiasi cha shilingi milioni mbili
alizipewa na MNEC zitasaidia katika ujenzi huo.
“Nimepewa pesa hizi na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Iringa (MNEC), Salim Asas nije niwaletee kwa niaba
yake hivyo nimezifikisha salama na nyie mzitumieni katika kumalizia ujenzi wa
nyumba hizo za walimu ili walimu waishi vizuri,” alisema Baraza.
Baraza alisema, Asas anapenda kuchangia maendeleo
katika sekta mbalimbali ndio maana katika shule hiyo amechangia zaidi ya mara
moja kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu katika shule hiyo.
“Mmesema
hapa wenyewe kuwa mara kadha amekuwa akiwasaidia kuchangia maendeleo katika
shule hii na leo kanituma niwaletee hizi pesa kwa ajili ya mchango wake kwenye
shule hii kwa lengo la kuboresha taaluma kwa wanafunzi wa hapa,” alisema Baraza.
Aidha
Baraza aliwataka wanafunzi wa shule hiyo kuhakikisha wasoma sana na kufaulu
mitihani iliyopo mbele yao na kurudisha fadhila kwa walimu na wazazi wao
waliowalea na kuwafundisha hadi hapo walipofika.
“Hakuna
kitu kizuri kwa mwanafunzi kufaulu mtihani na kusonga mbele hiyo maana walimu
wanawafundisha mkiwa shuleni lakini mkiwa nyumani wazazi wenu wanatumia gharama
kubwa kuwa somesha huku wakitegemea kupata matokeo chanya ya mtihani wenu wa
mwisho” alisema Baraza.
Baraza
aliongeza kwa kuwataka wanafunzi wa kidato cha sita kusimamia kikamilifu
malengo waliyojiwekea ili kuifikia ndoto ambayo wamekuwa nayo kwa miaka mingi
ya kupata au kufika maisha bora ambayo kila mwanadamu anatamani kuyafikia.
Lakini Baraza aliwapongeza walimu na wanafunzi
waliowahi kusoma shule hiyo kwa kupata matokeo mazuri kila mwaka na kusaidia
kukuza taaluma kwa wanafunzi wa shule hiyo na kuwaandaa vijana ambao watakuaja
kulisaidia taifa hapo baadae.
Awali
akisoma taarifa ya shule hiyo, Mkuu wa Shule, Laurent Manga alisema kuwa shule
hiyo inakabiliwa na changamoto ya umaliziaji wa nyumba ya walimu inayojengwa
kwa nguvu za wazazi,wanafunzi na serikali.
“Mgeni
rasmi sis hapa tunaupungufu wa bati mia moja na ishirini, saruji mifuko mia
tatu, mbao mia moja themenini na tisa pamoja na misumari kilo hamsini, hivyo ndio
vinakwamisha umaliaji wa nyumba hiyo ya walimu,” alisema Manga.
Manga alisema, uongozi wa shule uliweka malengo yake ya kuborsha makazi ya walimu kwa
kuanza kujenga nyumba tano ambazo mpaka sasa nyumba tatu zenye uwezo wa
kuhifadhi walimu sita zimekamilika na nyingine moja mafundi wapo kazini na ya
mwisho ikiwa hatua ya renta.
Hata hivyo Manga
alimalizia kwa kutoa shukrani kwa mjumbe
wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas
kwa mchango wake wa kimaendeleo ambao amekuwa akiufanya katika shule hiyo na
mahali pengine.
No comments:
Post a Comment