NA MWANDISHI WETU
VINARA wa huduma za kibenki
nchini, Benki ya NMB, wamezindua huduma ya kidijitali ya kuwawezesha Mawakala
wa NMB kupata mkopo wa salio la kuhudumia wateja ‘Floti Fasta,’ kupitia NMB
Mobile na NMB KLiK pindi wanapoishiwa salio.
Floti Fasta ni huduma ya uwezeshaji,
inayolenga kuwapa nguvu ya ziada mawakala wa NMB waliotapakaa kila kona, kupata
salio la dharura wanalohitaji kuhudumu nyakati za usiku ama wikiendi,
wanapokosa huduma za kuongeza salio katika matawi ya benki hiyo.
Huduma hiyo ya kwanza na ya
aina yake nchini, imezinduliwa mwishoni mwa wiki, ikilenga kukuza mitaji ya
mawakala, lakini pia kuwasaidia kukuza biashara zao, huku wakitengeneza ajira
kwa Watanzania wengi kupitia biashara zao za NMB Wakala.
Kiwango cha chini cha kupata
salio kupitia ‘Floti Fasta’ni Sh. 50,000 na kiwango cha juu ni Sh. Milioni 5,
huduma ambayo haina riba, bali mwombaji atatozwa asilimia 3 itakayojumuisha
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambako tozo litafanyika kabla ya mkopo
kutolewa.
Akizungumza wakati wa
kuzindua Floti Fasta, Mkuu wa Kitengo cha Malipo na Akaunti, Michael Mungure,
aliscma kuwa huduma hiyo, itawawezesha zaidi ya mawakala 6,800 kukuza biashara
zao na kuwapa uwezo wa kuhudumia wateja wao muda wote.
“Kupilia huduma hii ya Floti
Fasta, tatizo la kuishiwa salio kwa mawakala wetu limepatiwa ufumbuzi, Mteja
anatakiwa kutumia NMB Mobile au NMB KliK kuweza kupopa hususani kwa nyakati
ambazo hakuna huduma za kibenki kama usiku ama wikiendi,” alisema Mungure.
Mungure aliongeza kuwa:
“Dhamira yetu kila siku imekuwa ni kubuni bidhaa na huduma bora kwa kuangalia
changamoto mbalimbali za kifedha nchini na kuzipatia suluhu.
“Imekuwa wazi kuwa kuna
changamoto kubwa kwa mawakala ya kuishiwa floti na hivyo kusababisha wateja
kutopata huduma stahiki za kutoa na kuweka fedha hususani baada ya matawi ya
NMB kufungwa.
“Tulipoliona hili tukaona ni
fursa kubwa kutoa suruhisho la kifedha ambalo ni rafiki kwa mawakala kupitia
NMB Mobile na NMB KLiK,” alisisitiza Mungure.
Mawakala wa NMB wana mchango
mkubwa katika utoaji wa huduma za kifedha na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi
wa Taifa, ambapo Mungure amebainisha kuwa NMB ikiwa kama benki kubwa hapa
nchini, inaona umuhimu wa kuwasaidia mawakala wake ilikukidhi mahitaji ya soko.
“Kwa sasa, wateja wanaopata
huduma za kifedha kupitia NMB Wakala wana uhakika wa kupata huduma pasipo hofu
ya kukosa floti, kwani kupitia huduma hii, Mawakala wa NMB wanakuwa ndio wa
uhakika zaidi katika utoaji huduma za kifedha muda wowote na sehemu yoyote,”
alisema.
Mungure alisema kuwa, pamoja
na kwamba huduma hiyo imeanzishwa kwa ajili ya kuwasaidia mawakala wa NMB,
faida yake inakwenda mbali zaidi na kumfikia hata asiye mteja wa NMB, ambaye
ataweza kulipa Kodi za Serikali na bili kama za Dawasco, LUKU, muda wa maongezi
na kulipa ving’amuzi.
No comments:
Post a Comment