JIJI LA DAR LAOMBA TENDA KUTOA HUDUMA ZA USAFIRI KARIAKOO-MBAGALA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 12 March 2019

JIJI LA DAR LAOMBA TENDA KUTOA HUDUMA ZA USAFIRI KARIAKOO-MBAGALA

Mstahiki Meya Isaya Mwita

HALMASHAURI ya jiji la Dar es salaam imesema kuwa imepanga kuomba  zabuni ya utoaji huduma ya usafirishaji abiria kupitia mabasi yaendayo haraka kutoka Kariakoo Gerezani hadi Mbagala.
Kauli hiyo imetolewa jijini hapa leo na Mstahiki Meya Isaya Mwita mara baada ya kumalizika kwa kikoa cha baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee.
Meya Mwita amesema kuwa tayari Wakala wa mabasi yaendayo haraka wameshatangaza zabuni ya ujenzi wa awamu ya pili ya miundombinu ya mabasi itakayoanzia Kegerezani hadi Mbagala hivyo kama jiji limeona kunahaja ya kuomba zabuni hiyo ilikutoa huduma hiyo ya usafiri.
Amefafanua kuwa jiji linania ya kuomba zabuni hiyo kutokana na kuwa wanaweza kutoa huduma hiyo ili kusaidia adha ya foleni iliyopo kwa sasa katika maeneo ya Mbagala.
“  Tunatarajia kuomba zabuni ya kutoa huduma ya kusafirisha abiria hapa jijini ,iwapo tutakubaliwa basi kama jiji nalo litakuwa miongoni mwa watoa huduma hiyo” amesema Meya Mwita.
Tunajua kwamba pesa tunazo, nauwezo wakutoa huduma hiyo tunao,kwahiyo wakazi wa jijini hapa wafahamu kuwa kama tutakubaliwa tutatoa huduma hiyo, ndio mana leo nimewaeleza madiwani kwamba uliangalie jambo hili kwa umuhimu wake ilitujiandae” ameongeza.
Katika hatua nyingine baraza hilo limepitisha kwa kauli moja taarifa mbalimbali za utendaji na miradi mbalimbali zilizotolewa na wenyeviti wa kamati  mbalimbalimbali za jiji.

No comments:

Post a Comment