UJUMBE WA KATIBU MKUU WA UN KATIKA SIKU YA KIMATAIFA YA KUTOKOMEZA UKEKETAJI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 7 February 2019

UJUMBE WA KATIBU MKUU WA UN KATIKA SIKU YA KIMATAIFA YA KUTOKOMEZA UKEKETAJI

António Guterres


UKEKETAJI ni ukiukwaji wa haki za binadamu unaochukiza na ambao unadhuru wanawake na
wasichana kote duniani. Unawanyima utu wao, unahatarisha afya yao na kusababisha maumivu
yasiyo na sababu, hata kifo.

Ukeketaji umejikita katika kukosekana kwa usawa wa kijinsia na unaendeleza hayo kwa kuminya
fursa kwa wasichana na wanawake kutambua haki na uwezo wao kamilifu. Takribani wanawake
na wasichana milioni 200 walioko hai hii leo wameathiriwa na ukeketaji. Na kila mwaka takribani
wanawake milioni 4 wako hatarini kukeketwa.

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, yanatoa wito wa kutokomeza ukeketaji ifikapo mwaka
2030. Umoja wa Mataifa unaungana na juhudi za ulimwengu, kikanda na kitaifa katika kulifikia
lengo hilo. Kukabiliana na ukeketaji ni sehemu kubwa ya jitihada zetu katika mpango
uliozinduliwa kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya ili kukomesha aina zote za unyanyasaji
dhidi ya wanawake na wasichana.

Kutokana na utashi wa kisiasa, tunaona mabadiliko chanya katika nchi kadhaa. Hata hivyo ikiwa
mwelekeo wa sasa utaendelea, mafanikio yaliyopatikana yatazidiwa kasi na ongezeko la idadi ya
watu kwenye maeneo ambako mila hii potofu inatekelezwa.

Katika siku hii ya kutokomeza ukeketaji, ninatoa wito wa kuongeza hatua za kidunia za pamoja za
kutokomeza ukeketaji wanawake na kuzingatia kwa dhati haki za binadamu za wanawake na wasichana.

No comments:

Post a Comment