Naibu Waziri Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akitoa majibu ya Serikali kwa
maswali yaliyoelekezwa katika Ofisi yake juu ya masuala ya Muungano mapema hii
leo.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima
amesema kuwa Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ulianzishwa kwa lengo la kuchochea
maendeleo ya majimbo ya uchaguzi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ufafanuzi huo umetolewa hii leo katika kipindi cha
Maswali na Majibu wakati Mbunge wa Kiwani Mheshimiwa Abdalla Haji Ali alipouliza
swali kwa Serikali sababu ambazo hupelekea fedha za mfuko huo kuchelewa kufika
katika Majimbo ya Zanzibar.
Naibu Waziri Sima ameainisha
utaratibu unaotumika katika mgawanyo wa fedha hizo kutoka Wizara ya Fedha na
Mipango ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano; na jukumu la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania la kufanya mchanganuo wa kila Jimbo na kuwasilishwa Ofisi ya Makamu
wa Pili wa Rais Zanzibar ambayo huwasilisha Wizara ya Fedha na Mipango kwa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo Wizara ya Fedha na Mipango ya Zanzibar ndiyo
inayoingiza fedha kwenye akaunti za Majimbo ya Zanzibar.
“Hivyo, ni dhahiri
kuwa hatua hizo zinaweza kusababisha ucheleweshaji wa fedha hizo ukilinganisha
na fedha zinazopelekwa kwenye Majimbo ya Tanzania Bara. Hata hivyo, jitihada za
makusudi zinafanyika ili kuhakikisha fedha hizo zinaingia kwenye akaunti za
Majimbo ya Zanzibar kwa wakati”. Sima alifafanua.
Mchanganuo wa
mgawanyo wa fedha kwa kila Jimbo hutokana na vigezo vilivyoainishwa vya idadi
ya watu katika Jimbo, ukubwa wa eneo na kiwango cha umaskini, uchambuzi ambao
hufanywa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kuwasilishwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais, Zanzibar kwa utekelezaji.
Kuanzia mwaka 2010,
Ofisi ya Makamu wa Rais imeratibu na
kufuatilia Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo kwa upande wa
Zanzibar.
Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 16 ya Mwaka 2009 kwa lengo la kuchochea
maendeleo ya majimbo ya uchaguzi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment