Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi wakiwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Fonga,Mama Kimambo ,wajumbe wa serikali ya mtaa pamoja na Diwani wa kata jirani ya Bomambuzi Juma Raibu wakishuhudia namna ambavyo Bomba la maji limeunganishwa katika maungio ya Mita ili kufanikisha wizi wa maji.
Mwenyekiti w Serikali ya Mtaa wa Fonga ilipo shule ya Sekondari ya Anna Mkapa akitizama kwa karibu wizi wa maji ulivyofanyika katika shule hiyo.
Bomba likiwa limeunganishwa moja kwa moja mara baada ya kuondolewa Mita ya shule hiyo iliyokuwa ikitumika kuhesabu unit za maji yanayotumika katika shule ya Anna Mkapa.
Fundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) akifungua kipande cha Bomba kilichounganishwa kwa ajili ya kufanikisha wizi wa maji mara baada ya kuondoa Mita hiyo .
Na Dixon Busagaga, Moshi
SHULE ya Sekondari ya Anna Mkapa iliyopo kata ya Pasua
katika Manispaa ya Moshi imebainika kufanya udanganyifu kwa kushiriki kitendo cha kuiba Maji ya Mamlaka ya Majisafi na Mazingira mjini Moshi (MUWSA)
kinyume cha sheria.
Mbali na wizi huo wa maji uliofanywa na wahusika kwa
kuunganisha bomba katika maungio ya Mita za Maji pia Mamlaka imebaini kupotea
kwa Mita ya kusoma kiwango cha Maji kinachotumika iliyotolewa na MUWSA kwa shule
hiyo ambayo ilipaswa kuwepo katika Bomba hilo lililounganishwa kinyemela.
Tukio hilo lilibainika jana usiku majira ya saa 3:30 baada
ya wafanyakazi wa MUWSA kufanya operesheni ya kushtukiza katika shule baada ya
kupokea taarifa kutoka kwa wasamaria wema waliotoa taarifa kwa Mamlaka juu ya
wizi huo.
Akizungumza katika eneo la tukio ,Afisa Habari wa Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Rashid Nachan alisema kilichofanyika
ni wizi na kwamba wahusika wanachangia kuhujumu uchumi wa nchi.
“Kinachoonekana hapa dhahiri ni kwamba uongozi wa shule
unafahamu kinachoendelea ,kwa sababu hawezi kuja mtu kutoka nje kufanya kitendo
cha kutondoa Mita na kuweka Bomba la moja kwa moja bila uongozi wa shule
kufahamu ,atakuwa anafanya kwa faida ya nani sasa “alihoji Nachan.
Alisema kinachoonekana Shule ya Anna Mkapa imefanya kitendo
hicho kwa muda mrefu na kwamba kimekuwa kikifanyika majira ya usiku na ikifika
asubuhi hurudishia Mita kama kawaida mara baada ya Maji kujaa katika Matenki
yaliyopo shuleni hapo.
“Hatua tunazoenda kuchukua kwa sasa ni kufungua shauri Polisi
dhidi ya wahusika kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ikiwa ni pamoja na kufanya
mahesabu na kuandaa Bili ya kiasi cha
Maji yaliyoibiwa kwa muda wote “alisema Nachan.
Alipulizwa juu ya mada ya wizi wa maji ,Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Anna Mkapa ,Sindato Seiya alikiri kufanyika wizi wa maji katika
shule hiyo huku akitupi mpira kwa Mlinzi na Fundi wa miundombinu ya Maji wa
shule hiyo.
“Nimeiona sehemu yenyewe ,na toka jana usiku huyu fundi
ametafutwa na hapokei simu hadi sasa maana yake anajua mwenyewe ni kitu gani
amefanya,hapa shule kuna wafanyakazi wa asubuhi hadi saa tisa na anakabidhiwa
shule mlizni wa mchana ambaye pia anakabidhi kwa mlinzi wa usiku hao ndio
wanaweza kujua hili suala”alisema Mwl,Seiya.
Alisema yupo tayari kwa hatua zitakazochukuliwa kutokana na
kwamba yeye anafahamu wamekuwa wakilipa Bili za Maji kwa njia ya hundi kila
mwezi na kwamba wizi wa maji uliofanyika hajui wahusika wamefanya kwa faida ya
nani.
No comments:
Post a Comment