NMB YAKABIDHI MABATI, MADAWATI NA KOMPYUTA KWA SHULE NNE ZA DAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 1 February 2019

NMB YAKABIDHI MABATI, MADAWATI NA KOMPYUTA KWA SHULE NNE ZA DAR

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi (kulia) msaada wa kompyuta tano kwa ajili ya Shule ya Msingi Tandika iliyopo wilayani Temeke jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya walimu wakuu wa shule zilizonufaika na misaada hiyo.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi (wa pili kulia)  msaada wa mabati 200 kwa Shule ya Msingi Mabatini iliyopo wilayani Temeke jijini Dar es Salaam. Wengine kulia ni walimu wa Shule ya Msingi Mabatini wakishuhudia.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi (kulia) akiwapongeza baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Tandika mara baada ya kukabidhiwa msaada wa kompyuta zilizotolewa na Benki ya NMB.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mabatini, Bi. Victoria Joseph (kushoto) mara baada ya Benki ya NMB kukabidhi msaada wa mabati 200 kwa shule hiyo. Shule ya Msingi Mabatini inakabiliwa na uchakavu wa mabati na sakafu ya vyumba vya madarasa.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (wa pili kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi misaada hiyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi (kulia) akitoa shukrani kwa Benki ya NMB kwenye hafla hiyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mabatini, Bi. Victoria Joseph (kulia) akitoa shukrani kwenye hafla hiyo.

Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mabatini wakiwa katika hafla hiyo ya kupokea msaada.

No comments:

Post a Comment