Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe akizungumza na Watumishi wa Tasisi Mbalimbali za kifedha nchini. |
Na Humphrey Shao,
Wizara ya Fedha na Mipango kupitia
Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeandaa warsha kuhusu udhibiti wa utakasishaji wa fedha haramu na
ufadhili wa ugaidi kwa wadau wa sekta ya fedha kwa lengo la kuendelea kuwakumbusha
kuhusu umuhimu wa kulinda mfumo wa fedha
wa nchi yetu ili usitumiwe vibaya na wahalifu na watu wasio waaminifu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha
hiyo juu ya udhibiti wa utakasishaji wa
fedha haramu na ufadhili wa ugaidi, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo
cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe alisema tatizo la
utakasishaji wa fedha haramu ni tatizo kubwa ulimwenguni kote na katika jamii
kwasababu ya kuwepo kwa vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyowapatia wahalifu
pato haramu. Uhalifu huo ni pamoja na ukwepaji kodi, biashara haramu ya dawa za
kulevya, biashara haramu ya watu, biashara haramu ya silaha, rushwa, kughushi, ujangili,
uharamia, uvunaji haramu wa magogo, uuzaji wa bidhaa bandia, ujambazi na
uporaji n.k.
Aidha aliainisha madhara ya utakasishaji
wa fedha haramu kuwa ni ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiusalama. Madhara
hayo pamoja na uhalifu kuendelea kushamiri
kwa uhalifu na wahalifu kujiimarisha; wahalifu kuwa na nguvu kiuchumi; kuhatarisha utawala wa sheria na usalama (threaten
peace, stability and rule of law) kwani uhalifu unaposhamiri na makundi ya
uhalifu yanapojiimarisha hupata nguvu na kujaribu kudhibiti vyombo vya au
kushindana na vyombo vya dola; kuharibu ushindani (ruin competitiveness) wa
kibiashara katika uchumi kutokana na wahalifu kuwa na mitaji inayotokana na
fedha haramu, wafanyabiashara halali hushindwa kuhimili ushindani; kushusha
hadhi ya nchi kimataifa (erosion of country’s integrity) na kusababisha nchi
kutonufaika na mfumo wa fedha wa kimataifa; kushusha imani ya wawekezaji na
kusababisha uwekezaji kupungua na wawekezaji wapya kutotaka kuwekeza kutokana
na kushamiri kwa uhalifu, wawekezaji huwa na hofu kuwa mitaji na mali zao havitakuwa
salama; imani ya washirika wa maendeleo na jumuiya ya kimataifa hupungua na nchi huathirika kiuchumi; kushuka kwa hadhi ya taasisi za fedha na mfumo mzima wa fedha; na nchi kushindwa kufikia
malengo ya maendeleo kwani rasilimali huwa mikononi
mwa wahalifu wachache badala ya kutumika kutekeleza ajenda pana ya maendeleo ya
nchi.
Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti
Fedha Haramu amewaasa na kuwakumbusha washiriki wa warsha hiyo kuendelea
kushirikiana na taasisi mbalimbali kutekeleza wajibu wao wa kisheria kwa
uadilifu na uaminifu ili kuendelea kusaidia katika kubaini wahalifu wanaoweza kutumia
mfumo wa fedha wa nchi kutakasisha fedha haramu na kufadhili vitendo vya
kigaidi na kuhatarisha usalama wa nchi.
Warsha hiyo imejumuisha washiriki
kutoka benki na taasisi zinazotoa huduma za kibenki na huduma ndogo ndogo za
fedha.
Kamishna Msaidizi ,Huduma za Kompyuta Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Gilbert .R.Nyombi akizungumza na Watumishi wa Tasisi Mbalimbali za kifedha nchini alipokuwa akitoa mada juu ya kudhibiti fedha haramu.
Baaadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo wakifatilia mada zilizokuwa zikitolewa na Mtaalamu kutoka FIU Kwa umakinimu.
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika Picha ya Pamoja na AmuKamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe.
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika Picha ya Pamoja na AmuKamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe.
No comments:
Post a Comment