Mkurugenzi mkazi wa taasisi inayojishughulisha na maswala ya kisaikolojia (RESPSSI) Tanzania,Edwick Mapalala akizungumza wakati wa kampeni ya kutomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni.
Mkurugenzi mkazi wa taasisi inayojishughulisha na maswala ya kisaikolojia (RESPSSI) Tanzania, Edwick Mapalala akizungumza wakati wa kampeni ya kutomeza tatizo la ndoa na mimba za utotoni.
Baadhi ya vijana wa boda boda waliochangia mjadala wa kupinga ndoa na mimba ya utotoni.
Na Mwandishi, Mkuranga
SHIRIKA lisilo la Kiserikali linalojihusisha na msuala ya
Kisaikolojia nchini (REPPS) limeanza kufanya kampeni ya kupambana na tatizo la
mimba na ndoa za utotoni baada ya tafiti nyingi kuonyesha bado tatizo hilo ni
kubwa.
Takwimu za Democratic
and Health Survey , zinaonyesha kuwa tatizo la mimba za utotoni nchini
limeongezeka kutoka asilimia 23 mwaka 2010 hadi kufikia 27 mwaka 2016/17,
kutokana na ukosefu wa huduma pamoja na elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenye
umri kuanzia miaka 15 hadi 19.
Mkurugenzi Mkazi wa
Repps, Tanzania Edwick Mapalala amesema kampeni hiyo wanaiendesha kwa
kuzungumza na jamii kwenye vijiwe, shambani, maeneo ya masomo na mikusanyiko
yote ili kufikisha elimu ya namna ya kuwalea na kuwatunza watoto kimaadili.
“Tatizo la mimba na
ndoa za utotoni lipo kwenye jamii yenyewe, wazazi na walezi wakijua umuhimu wa
malezi bora tatizo hili halitakuwepo kabisa,” amesema.
Amesema kama watoto wa
kike wataendelea kukatisha masomo yao kwa mimba na ndoa itakuwa vigumu kufikia
ndoto ya Tanzania yenye viwanda kwa sababu nguvu kazi inayoachwa njiani ni
kubwa.
“Mtoto wa kike akipata
elimu na kusoma kwa bidii atatimiza ndoto yake na kuja kuchangia maendeleo
kwenye taifa lake,” amesisitiza.
Amesema kupitia
kampeni hiyo wanayoiendesha kwa ushirikiano na Shirika lililo chini ya Kanisa
la Roman Katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam (PASADA), vijana wameweza kupewa
elimu ya afya ya uzazi na kujitambua itakayowasaidia kufikia ndoto zao.
Kaimu Afisa Mtendaji
wa Kijiji cha Parang’andam Felisian Magulu amesema kupitia kampeni hizo jamii
inapata ufahamu wa madhara ya mimba kwa watoto na kujua namna ya kupambana na
tatizo hilo.
Naye Mwenyekiti
wa Kijiji cha Mkuranga, Dunia Mabufu alikiri kuwepo kwa kampeni za aina hiyo
kunasaidia katika kubadilisha fikra za wengi zinazoendeshwa na mila na desturi
kandamizi dhidi ya wasichana na wanawake.
No comments:
Post a Comment