WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI KUJADILI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA JIJINI DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 12 November 2018

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI KUJADILI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA JIJINI DODOMA

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Frolens Luoga, nje ya viwanja vya Bunge, Jijini, Dodoma, baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kujadili  Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni siku chache zijazo.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. David Silinde (Mb), akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kijitabu cha Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha, wakati kamati hiyo ilipokutana na Waziri huyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi (Mb)  na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, kujadili Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, utakaowasilishwa kwa hati ya Dharura katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Andrew Chenge (Mb) na Prof. Anna Tibaijuka (Mb) wakifuatilia kwa makini mjadala wa Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Bungeni, Jijini Dodoma, siku chache zijazo.

No comments:

Post a Comment