BREAKING NEWZ: SERIKALI YAFUNGA MJADALA, KUNUNUA KOROSHO YENYEWE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 12 November 2018

BREAKING NEWZ: SERIKALI YAFUNGA MJADALA, KUNUNUA KOROSHO YENYEWE

Rais John Pombe Magufuli akizungumza.

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli leo amemaliza mjadala wa ununuzi wa zao la korosho mikoa ya kusini, baada ya kulikabidhi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuilinda na kuisafirisha kwenda kwenye maghala makubwa na viwanda vitakavyo ibangua kabla ya kutafutiwa masoko. 2 na naibu 4

Katika maelekezo yake jijini Dar es Salaam akiwaapisha mawaziri wapya, amesema muda aliotoa kwa wanunuzi binafsi umeisha na sasa korosho yote itanunuliwa na Serikali kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini kutoa zitakozotumika kununua korosho toka kwa wakulima kwa bei ya sh 3,300 kwa kilo. Akifafanua zaidi alisema usafirishaji na ulinzi katika maghala yote ya kuifadhi korosho utafanywa na JWTZ na sasa tayari wapo kazini kutekeleza agizo hilo.

Kwa agizo hilo kwa sasa hakuna mtu au kampuni yoyote itakayoruhusiwa kununua korosho kutoka kwa wakulima zaidi ya Serikali na vyombo vyake husika na itaibaangua na kuitafutia masoko nje na ndani ya nchi.

"...Tumechezewa sana na wanunuzi binafsi, wanawanyanyasa wakulima wetu...Serikali haiwezi kuvumilia vitendo kama hivi, lazima tuwalinde wakulima wetu. Benki ya Maendeleo ya Kilimo toeni fedha wakulima walipwe fedha zao 'cash' tutainunua korosho na kuitafutia soko wenyewe baada ya kuibangua na tukikosa hata wenyewe (Watanzania) tutakula," alisema Rais Magufuli.

Mawaziri wapya walioapishwa ni Japhet Ngailonga Hasunga kuwa Waziri wa Kilimo na Joseph George Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Manaibu waziri wengine walioapishwa leo ni Constantine John Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mwita Mwikwabe Waitara kuwa Naibu Waziri wa TAMISEMI na Innocent Lugha Bashungwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Uteuzi wa viongozi hao ulianza Novemba 10, 2018 baada ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kuwatumbua Waziri wa Kilimo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji kufuatia sakata la korosho.

 

No comments:

Post a Comment