KATIKA kuunga mkono lengo la serikali la
kupunguza vifo vya uzazi na watoto njiti kwa kupunguza uwiano wa vifo vya
uzazi hadi kufikia watoto 292 kati ya watoto 100,000 kwa vizazi hai
kutoka watoto 556 kati ya 100,000 ifikapo mwaka ....., Vodacom Tanzania
Foundation ikishirikiana na Doris Mollel Foundation imetoa mchango wenye
thamani ya TZS 25 milioni kwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ili kulinda maisha
ya watoto njiti.
Tukio hili lilishuhudiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Waziri wa Madini
mheshimiwa Angellah Kairuki, na Mheshimiwa Antony Mavunde Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu.
Msaadawetuunajumuisha vifaa muhimu vya kuokoa
maisha kama vile vifaa vya oksijeni (Oxygen concentrator) ambavyo vitasaidia
watoto njiti kupumua, thermometers 10, 4 weighing scales for infants, 40
branded bedsheets, baby warmer, 3 suction machines, ambu bag with facemasks for
infants, 1000 feeding tubes, phototheraphy machine, na vitanda vitatu vya
watoto. Mchango kama huo pia
utawasilishwa katika Kambi ya Wakimbizi iliyoko Nyarugusu Mkoani Kigoma.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Kitengo
cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom, Bi Rosalynn Mworia alisema,
"Vodacom imeazimia kupunguza idadi ya vifo vinavyotokea wakati wa
kujifungua pamoja na vifo vya watoto wachanga na inaunga mkono jitihada za
serikali za kuboresha utoaji wa huduma za afya. Tunatarajia kwamba mchango wetu
utaenda mbali katika safari nzima ya kuokoa maisha mengi zaidi ya wanawake na
watoto. "
Kwa upande wake, Mheshimiwa Ummy Mwalimu alisema,
"Mpango huu unakuja wakati muafaka ambapo serikali imeanza kampeni ya
kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na watoto wachanga
hapa nchini. Tunapenda kuwashukuru Vodacom Foundation na Doris Mollel
Foundation katika kusaidia nchi kukabiliana na changamoto hizi. Vifaa hivi
cheza nafasi muhimu katika kukabiliana na matatizo ambayo watoto njiti hukutana
nayo hasa katika wiki nne za kwanza za maisha yao."
Alitoa wito kwa wafanyakazi wa afya kuhakikisha matumizi
sahihi ya vifaa vya kuokoa maisha ya watoto njiti akisema, "Ninawasihi
wafanyakazi wa afya katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kutumia kwa usahihi
vifaa hivi. Msiruhusu mashine zikusanye vumbi, mashine hizi ziko hapa kwa ajili
ya kuokoa maisha ya Watoto wetu. "
Pia alikuwepo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge
ambaye alisema kupambana na vifo vya watoto wachanga nchini Tanzania ni suala
mtambuka, maana ni wajibu wa kila mmoja wetu kwa pamoja. "Mchango huu ni
ishara kubwa ya ushirikiano kwa kampeni inayoendelea, Jiongeze - Tuwavushe
Salama na inalingana na kiapo nilichochukua, pamoja na Wakuu wengine wa Mikoa,
ambapo tuliahidi kufanya kazi ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga
nchini Tanzania kwa mujibu wa mkakati husika wa serikali chini ya Wizara
ya Afya. "Alisema.
Kwa upande wao, Mheshimiwa Angela Kairuki, na Mheshimiwa
Antony Mavunde, waliihimiza Vodacom Tanzania Foundation kuendelea na jitihada
za kusaidia wanawake na wasichana nchini kote kuboresha afya zao, kupata elimu
bora na kubuni miradi mipya.
No comments:
Post a Comment