Abdallah Mtolea |
MBUNGE wa TEMEKE (CUF), Abdallah Mtolea amejivua uanachama na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani ya CUF akidai kumekuwa na migogoro mingi ndani ya chama chake. Mtolea ametangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma hii leo Novemba 15, 2018.
Baada ya kumaliza kutangaza kujiuzulu, Mtolea alitoka nje ya Ukumbi wa Bunge na kuondoka bungeni hapo.
Taarifa hizo zimethibitishwa pia na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ambaye amesema amepokea barua ya kujiuzulu kwake.
Mbunge huyo amevialika vyama vingine vya siasa nchini kufanya naye kazi akidai bado anatamani kuendelea kuwatumikia wananchi wa Temeke.
No comments:
Post a Comment