WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama amefanya ziara ya siku moja mkoani Dar es salaam, lengo la ziara hiyo
ni kukagua miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko pamoja na kutaka
kujua mikakati ya kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa mkoani humo ya
kukabiliana na maafa hayo.
Katika ziara hiyo
Waziri Mhagama emetembelea wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam hususan katika
maeneo ambayo mkoa huo umeboresha miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko.
Maeneo hayo ni Jangwani, Mto Mbezi, Mto Ng’ombe, Mto Bungoni na mfereji wa
Mtoni kwa Azizi Ally.
Pamoja na kuridhishwa
na jitihada zilizofanywa na mkoa wa Dar es salaam za kuboresha miundombinu ya
kukabiliana na maafa ya mafuriko, pia na mikakati ya kukabiliana na maafa hayo
waliyomueleza, Waziri Mhagama ametoa maagizo 5 kwa kamati ya Usimamizi wa menejimenti
ya maafa ya mkoa huo kuyatekeleza ili
menejimenti ya maafa ya mafuriko mkaoni Dares salaam iwe endelevu.
“Nimeridhishwa
na juhudi zilizofanywa na serikali kuu chini ya uongozi wa Dkt.Joh Pombe
Magufuli za kuboresha miundo mbinu ya kakabiliana na maafa ya mafuriko, na
nimeona jinsi serikali ya ngazi ya mkoa na wilaya zote zinavyo jitahidi kujenga
uwezo wa kuzuia, kujiandaa na
kukabiliana na maafa. Pamoja na jitihada hizo ninge penda kuishauri na kuielekeza kamati na Mkuu wa mkoa
ayasimamie maelekezo yangu.” Amesisitiza Mhagama.
Mhagama ameiagiza
Kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa kusimamia suala la uharibifu wa
mazingira hususani maeneo ya mito na mabondeni kwa mujibu wa sheria ya
menejimenti ya maafa ya mwaka 2015. Aidha alifafanua kuwa Maafa mengi ya
mafuriko mkoani humo yanatokana na uharibifu wa mazingira unaochangiwa na ujenzi
katika maeneno yasiyo stahili kama kingo za mito na mabondeni hali
ambayo huzuia maji kutiririka na kusababisha mafuriko.
Aidha Mhagama ameitaka
kamati hiyo kusimamia suala la usafi wa
mitaro, mifereji na mito iliyopo
jijini Dares salaam, ambayo hujaa
maji wakati wa msimu wa mvua kutokana na
uchafu na takataka zilizotupwa katika mifereji na mitaro hiyo hali ambayo
husababisha maji kushindwa kutirirka kuelekea baharini na hatimaye mitaro hiyo
hujaa na kusababisha mafuriko.
Ameitaka kamati hiyo
kuwasiliana na sekta nyingine zenye miundmbinu katika mitaro na mifereji inayojengwa
na kuondoa miundo mbinu hiyo ili uboreshaji wa miundo mbinu hiyo kuwa wa
ufanisi. Mhagama alibainisha kuwa Mkoa umefanya
juhudi nzuri za kujenga mitaro na mifereji lakini ndani ya miundo mbinu hiyo kuna miundombinu mingine kama vile mabomba
ya maji safi, hivyo,
sekta nyingine husika hazina budi kushrikishwa na kuhakikisha miundo
mbinu hiyo inatolewa ili kulifanya zoezi la kuboresha miundombinu ya maafa ya
mafuriko linakuwa bora na ufanisi.
Kamati imetakiwa
kuhakikisha miradi yote inayolenga kuboresha miundombinu ya kukabiliana na
maafa ya mafuriko ndani ya mkoa wa Dar es salaam inashirikiana katika hatua ya
kupanga utekelezaji wake. Mhagama amefafanua kuwa Mkoa una miradi mingi ya
kuboresha miundo mbinu ya kukabiliana na maafa hivyo ni vyema miradi hiyo ikae
pamoja ili kujua ni namna gani ya kutekeleza malengo yake hususani kujua miundo
mbinu husika inawekwa wapi bila kuathiri utekelezaji wa mradi mwingine.
Mhe.Mhagama ameitaka
kamati kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya sheria ya menejimenti ya maafa ya
mwaka 2015. Amebainisha kuwa kila mmoja katika jamii analojukumu la kuzuia,
kujiandaa na kukabiliana na maafa, hivyo jamii ikiwa na elimu ya kutosha juu ya
menejimenti ya maafa hususani ya mafuriko jamii haitapata athari kubwa za uharibifu
wa mali na vifo vitokanavyo na maafa ya
mafuriko.
Awali akieleza mikakati iliyopo ya
kukabibiliana na maafa katika mkoa wa Dar es salaam, Mkuu wa mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda alifafanua kuwa mkoa wa Dar es salam umekuwa ukitumia
fedha nyingi wakati wa kurejesha hali ya miundo mbinu iliyoathirika kutokana na
maafa ya mafuriko ambapo kwa mwaka 2011, kiasi cha shilingi bilioni Nne na nusu
kilitumika kurejesha hali ya miundo mbinu ya barabara iliyoharibika.
“Mkoa wa Dar es salaam
tuna mito mikubwa saba ambayo inatiririsha maji
kuelekea baharini, na mito midogo midogo mingi, sisi kama mkoa
tumejipanga kuhakikisha mito hiyo ambayo hujaa maji na kusababisha maafa ya
mafuriko tunaidhibiti. Kupitia Benki ya Dunia tunao mpango wa kuchukua picha za
anga la mkoa wa Dar es salaam, lengo ni kujua nyumba zilizo kando ya mito
hiyo na idadi ya mito na kujipanga jinsi
ya kuhakikisha kuwa haileti athari ya mafuriko”amesema Makonda.
Naye mwenyekiti wa
Kamati ya Usimamizi wa Menejimenti ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mujibu
wa sheria ya maafa ya menejimenti ya maafa mwaka 2015, Katibu Tawala wa mkoa wa
Dar es Salaam, alimhakikishia Waziri Mhagama kutelekeleza maagizo hayo kwa
wakati kwa kuwa tayari kamati ya Usimamizi wa menejimenti wa maafa ya mkoa imesimamaia
uundwaji wa kamati za Usimamizi wa menejimenti ya maafa katika Halmashauri zake
tano hai itakayo saidia ufuatiliaji wa masuaa ya maafa mkoani humo.
Katika ziara hiyo
Waziri Mhagama aliambatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na
Uratibu), Profesa. Faustin Kamuzora,
Mkurugenzi wa Idara ya uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy
Matamwe, Mkuu wa wila ya Ilala, Temeke, na Kinondoni pamoja na wajumbe wa
Kamati ya Usimamizi wa Menejimenti ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILINO
SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU
No comments:
Post a Comment