TMA YAPONGEZWA KWA UBORESHWAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP
.com/img/a/

Tuesday, 15 April 2025

demo-image

TMA YAPONGEZWA KWA UBORESHWAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA

 WhatsApp%20Image%202025-04-15%20at%2020.37.53_9896cd3a

WhatsApp%20Image%202025-04-11%20at%2015.02.09_749d8d88


WhatsApp%20Image%202025-04-15%20at%2020.38.05_b0a6d916

WhatsApp%20Image%202025-04-15%20at%2020.38.04_59788d9c

WhatsApp%20Image%202025-04-15%20at%2020.38.01_81a00a4b

WhatsApp%20Image%202025-04-15%20at%2020.38.00_655ba073

WhatsApp%20Image%202025-04-15%20at%2020.37.56_a991dede

WhatsApp%20Image%202025-04-15%20at%2020.37.56_79121ee7

WhatsApp%20Image%202025-04-15%20at%2020.37.55_5289e982

WhatsApp%20Image%202025-04-15%20at%2020.37.53_f31251a7


WhatsApp%20Image%202025-04-11%20at%2015.06.38_60c77b92

WhatsApp%20Image%202025-04-11%20at%2015.02.31_a1ccea49


WhatsApp%20Image%202025-04-11%20at%2015.00.52_22c3b4fe

WhatsApp%20Image%202025-04-11%20at%2015.00.51_1b59916e

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imepongezwa kwa uboreshwaji wa utabiri wa hali ya hewa na taarifa za tahadhari za matukio ya hali mbaya ya hewa nchini. Hayo yamesemwa na Mhe. Dkt. Rozalia Rwegasira,  Kaimu Katibu Tawala Mkoa, sehemu ya uchumi na uzalishaji wa mkoa wa Morogoro wakati wa ufunguzi wa Semina ya Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Jamii Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa na matukio ya Hali Mbaya ya Hewa, kwaajili ya Kupunguza Hasara na Uharibifu ,iliyofanyika mkoani Morogoro katika ukumbi wa NSSF, tarehe 15/4/2025.

“Utabiri wa hali ya hewa umeendelea kuboreshwa na tahadhari za mvua kubwa na matukio ya hali mbaya ya hewa zinatolewa kwa wakati na hivyo kuchangia kuokoa maisha ya watu na mali zao. Tunaishukuru na kuipongeza serikali kwa kupitia TMA kwa kazi hii njema”. Alisema Dkt. Rozalia.

Aidha, Dkt. Rozalia alitoa ahadi ya kushirikiana na TMA katika kufanikisha utekelezwaji wa mradi huu kwani utakuwa na faida kubwa na chanya kwa wananchi wa Tanzania.

“Katika kufanikisha utekelezaji wa Mradi huu, kwa niaba ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa tuanaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha kwamba wananchi wananufaika na taarifa  zitakazozalishwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia Mradi huu, ili wadau na wananchi kwa ujumla kuweza kuchukua tahadhari kwa lengo la kupunguza athari zitokanazo na matukio ya hali mbaya ya hewa”.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA ambaye ni Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Hali ya Duniani (WMO) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a aliishukuru Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya hali ya hewa nchini.

“Nitumie fursa hii kutoa shukurani zangu za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuwekeza na kuisaidia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika kuimarisha huduma za hali ya hewa nchini kwa kuweka sera, mikakati na mazingira wezeshi yanachochea ubunifu na umahiri".

Dkt. Chang’a alisisitiza kwamba uwekezaji wa serikali kwenye miundombinu ya hali ya hewa nchini ndio chanzo kikuu cha uboreshwaji wa taarifa za hali ya hewa nchini na kuwasisitiza wananchi kuendelea kufuatilia  na kuzingatia taarifa za utabiri na tahadhari zinazotolewa na TMA, na pia kuzingatia sheria  ya Mamlaka ya Hali ya Hewa namba 2 ya mwaka 2019 na kanuni zake.

Mamlaka ya Hali ya Hewa inatoa shukrani za dhati kwa Tume ya sayansi na teknolojia (COSTECH) kwa kufadhili mradi huu muhimu ambao utaongeza ufanisi katika mchakato wa kukabiliana na mabadiliako ya hali ya hewa  na tabianchi nchini.

Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *