NMB YADHAMINI HAFLA YA KAMPUNI BORA 100 MWAKA 2018/2019 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 22 October 2018

NMB YADHAMINI HAFLA YA KAMPUNI BORA 100 MWAKA 2018/2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza kwenye hafla ya kutunuku kampuni Bora ya mwaka 2018/2019 (Top 100 Mid-sized Companies' Survey).

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akisalimiana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harison Mwakyembe kwenye hafla hiyo.

Meza kuu katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) katika mazungumzo na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harison Mwakyembe (katikati) kwenye hafla hiyo.


KAMPUNI Bora 100 Tanzania (Top 100 Mid-sized Companies' Survey) ni shindano linaloendeshwa na Mwananchi Communications Limited kwa kushirikiana na KPMG. Shindano hili ambalo hufanyika kila mwaka tangu 2011, huku likiwa na lengo la kuzitambua na kuzizawadia kampuni za kati zinazofanya vizuri, kuchochea maendeleo ya Tanzania kiuchumi.

Benki ya NMB ni miongoni mwa wadhamini wa shindano hili, huku ikijikita katika kusaidia eneo la SME, kipengele ambacho ni muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kuchochea makampuni hayo kufanya vizuri zaidi.

NMB ni kichocheo muhimu cha SME pia, lazima ijenge mazingira mazuri ili kuleta maendeleo zaidi. Utafiti huu kwa makampuni ni muhimu kwa sababu unatoa jukwaa la SMEs, kampuni ambazo wengi ni wateja wetu, kupata mafanikio katika maendeleo ya kiuchumi na taifa kwa ujumla.

Makampuni ambayo yanaingia katika ushindani ni yale ambayo mauzo yao yanaanzia shilingi 1 za kitanzania hadi bilioni 20, na kumbukumbu zake za kifedha kukaguliwa kwa miaka 3 iliyopita, na pia isewe kwenye orodha ya soko la hisa wala kuwa kampuni ya benki / bima / SACCOS / Sheria / Uhasibu au kampuni ya ukaguzi mahesabu. 

Makampuni za Juu 100 zilizopitishwa kati za makampuni yote yaliyoshiriki yatazingatiwa katika ukuzaji kimapato.

Mbali na NMB, wengine wa kampuni bora Bora ya mwaka 2018/2019 ni pamoja na Soko La Hisa la Dar es Salaam na Azam Media na Hoteli ya Hyatt Regency.

No comments:

Post a Comment