Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ziara yake mkoani Pwani alipotembelea mradi wa tenki la kuhifadhia maji linalojengwa katika wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita Milioni sita za maji.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Pwani, wakiwa katika eneo la mradi wa tenki l Maji katika wilaya ya Kisarawe ambalo linajengwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Makame Mbarawa akitoa taarifa juu ya Miradi mbalimbali ya maji inayoendelea hivi sasa ikiwa na lengo la kuondoa chanagmoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais ,Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara katika wilaya ya Kisarawe Mapema.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mogelo akifanya utamburisho wa wageni wakati wa ziara hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuonesha Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia ramani, maeneo ambayo mradi wa maji kutoka tenki la Maji la Kibamba hadi Kisarawe utapita.
Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe akimueleza jambo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Makame Mbarawa akizungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Sehemu ya ujenzi wa tenki hilo unavyoonekaana katika wilaya ya Kisarawe.
Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Prof Makame Mbarawa mara baada ya kutembelea eneo hilo la mradi wa tenki la Maji.
Na Dixon
Busagaga, Kisarawe.
MAKAMU wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu ameimwagia sifa
Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Waziri wake, Makame Mbarawa kwa utendaji wake
wa kazi nzuri inayofanya kwa kasi ili kuhakikisha huduma ya maji inapatikana
kwa uhakika.
Mbali na
Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mama Samia pia ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya
Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa hatua kubwa wanayoifanya ya
kutimiza azma ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama katika mkoa wa Pwani .
Makamu wa
Rais ametoa pongezi hizo leo alipotembelea Mradi wa tenki la Kuhifadhia Maji
yatakayosukumwa kutoka Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu kupitia tenki la Maji la
Kibamba ,mradi ambao utagharimu zaidi ya Sh Bilioni 10.4 huku akiwataka
wananchi wa Kisarawe kulinda miundo mbinu ya maji.
Amesema awali kulikuwa na tabia kwa miradi
kusuasua na kwamba kwa usasa chini
ya usimamizi wa Waziri Mbarawa Miradi hiyo itaenda vizuri na maji yatapatikana.
"Kuja
kwa mradi huu mkubwa wa maji utawapatia vijana ajira katika viwanda baada ya
wawekezaji kuja na najua umeme upo na wa gesi unakuja," amesema Mama Samia.
Kwa upande
wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amesma mradi huo unajengwa chini ya kampuni ya Chico
na utadumu kwa miezi minane na kwamba hadi kufikia Julai 2019 utakuwa
umekamilika ikiwa ni pamoja uwekaji wa bomba la Km 5 kwenda Vigungu na Km 14
kwenda Viwandani,
“Katika kutekeleza
miradi mbalimbali, DAWASA imetengwa akaunti maalumu ambapo asilimia 35 ya mapato inawekwa kwenye akaunti hiyo kwa
ajili ya kuendesha miradi mbalimbali.na kwa mradi huu mbali na ujenzi wa tenki
la kuhifadhi maji pia zitafungwa pampu nne kubwa kwa ajili ya kusukuma maji kwa
wananchi wa Kisarawe," alisema Mbarawa.
Naye Waziri
wa TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo ameshukuru kwa mradi wa maji
kufika Wilaya ya Kisarawe na kupitia mradi huu wana kisarawe watakuwa
wamenufaika kwa asilimia kumi.
Ameyataja
maeneo ya Mzenga na Mwanalumango kuwa na shida kubwa ya maji na watu wa
Kisarawe wanaishukuru sana serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John
Pombe Magufuli kwa kufanikisba mradi huu kwani ni mara ya kwanza toka kupata
kwa uhuru.
No comments:
Post a Comment