Na Ahmed Mahmoud, Monduli
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa. Loota Sanare amesema kuwa kampeni za chama hicho kwenye chaguzi za marudio ni salamu kwa wapinzani kwani wao wanajaribu mitando yao kabla ya kuingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani.
Ameyasema hayo kwenye Kampeni za chama hicho kwenye Mji wa Mto wa Mbu mapema juzi na kuongeza chama hakitamuonea haya mtu yeyote atakayeenda kinyume na misingi kanuni na taratibu za chama na hawatasita kunyang’anya kadi yao.
Amesema kuwa CCM ni chama chenye kufuata misingi na sheria kwa ajili ya kuwatumikia watanzania hivyo yeyote atakayepewa nafasi na chama hicho anawajibu wa kuwatumikia wananchi nasi kinyume na hivyo kwani tumekuja kwenu kuomba ridhaa tukiweka mkataba nanyi kushughulikia kero zenu.
“Ndugu zangu wakazi wa Wilaya ya Monduli tumekuja kuomba ridhaa kwenu mumpitishe mgombea wetu akienda kinyume na kanuni taratibu za kuwatumikia wanyonge hatutasita kumuwajibisha hii ndio CCM ya wanyonge na watu wote,” alisema Sanare.
Kwa upande wake Meneja kampeni hizo, Wiliam Ole Nasha ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu Sanyansi na Teknolojia amesema ushindi wa CCM wilayani humo upo wazi na kuwataka wananchi kwenda kumpigia kura mgombea wa chama hicho Julius Kalanga ili akamalizie sehemu iliyobaki ya kero zao.
Amesema kuwa misingi iliyowekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo inampa kiburi cha kusema kuwa CCM itashinda tena kwa kishindo katika uchaguzi wilayani hapa.
“Serikali ya CCM chini ya Dkt.John Magufuri imejipambanua wazi kuwatumikia wayonge ndio maana unaona wengi wanatoka upinzani kuja kuendeleza mazuri aliyoyafanya Mh. Rais na Mwenyekiti wa Taifa wa chama chetu hivyo ushindi hapa ni lazima,” alisema Ole Nasha.
Naye Mgombea wa chama hicho Julius Kalanga alisema kuwa hao sababu itakayomzuia kupata ushindi kwenye uchaguzi huo na kuendelea kuahidi kushughukia kero za wananchi wa jimbo hilo kwa nguvu zote na ushirikiano kutoka kwa wananchi hao.
Amesema yeye ni mtumishi wa wananchi na kipimo chake ni siku ya kupigiwa kura ila anaamini wananchi wa Monduli wamemuelewa na wataonyesha kwa vitendo siku ya uchaguzi huo 16/9/2018 kwani maneni sio kazi bali ni sehemu ya kufikia maelengo ya kazi.
Akatanabaisha kuwa yeye hakutoka upinzani kwenda Chama Cha Mapinduzi kwa kufuata fedha bali ilikuwa ni kurudisha heshima kwa wananchi waliomchagua kwa kufanyiakazi kero zao na matatizo yao ilikufikia maendeleo ya kweli ndani ya Wilaya ya Monduli.
“Nawasihii sana muwaonyeshe kuwa heshima yenu imelindwa na Chama Cha Mapinduzi kwani lengo letu ni umoja na mshikamano wetu hatimaye ushindi wa kishindo,” alisisitiza Kalanga
Kampeni za CCM zinaendelea jana kwenye kata ya Makuyuni nje kidogo ya Mji wa Monduli ambapo siku ya Jumapili kampeni hizo zitakuwa kwenye Kata ya Mswakini.
No comments:
Post a Comment