Wagombea uchaguzi wa Zimbabwe. |
Kiongozi huyo muanzilishi, Mugabe alitimuliwa katika mapinduzi
mwaka jana baada ya kuwa madarakani kwa takriban miongo minne.
Wagombea wakuu katika uchaguzi wa urais ni kiongozi aliyepo
Emmerson Mnangagwa,wa chama tawala Zanu-PF na kiongozi wa upinzani Nelson
Chamisa.
Uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa pia zinafanyika leo
Jumatatu.
Kura za kutafuta maoni zinampa uongozi mdogo Mnangagwa, mwenye
miaka 75, dhidi ya mpinzani wake mwenye miaka 40 anayekiongoza chama cha Movement
for Democratic Change (MDC).
Hapo jana kiongozi wa zamani
Robert Mugabe - aliyeingia kwa mara ya kwanza madarakani mnamo.
Kunashuhudiwa idadi kubwa ya watu wanaopiga kura kwa mara ya
kwanza nchini , ambako kura ya vijana ndio inayotazamwa kuwa na uzito. Takriban
nusu ya watu waliosajiliwa kupiga kura wapo chini ya miaka 35.
Mamia ya waangalizi wametumwa kuhakikisha uchaguzi unakwenda
sambamba, lakini mara kwa mara upinzani umetuhumu kuwepo udanganyifu katika
daftari la wapiga kura.
Wameelezea wasiwasi pia kuhusu usalama wa makaratasi ya kupiga
kura na kunyanyaswa kwa wapiga kura hususan katika maeneo ya mashinani.
Uchaguzi huo unafuata miongo kadhaa ya utawala wa unyanyasaji
uliosababisha changamoto kubwa za kiuchumi kwa taifa hilo.
Hili linajumuisha masuala ya uwekezaji, elimu, afya na ajira -
takwimu kadhaa zinaashiria kwamba ukosefu wa ajira upo juu kwa 90%.
Rais Mnangagwa, anayejulikana kama "Mamba" ameahidi
kuhakikisha kuna nafasi za ajira na anaonekana kukubali kuidhinisha mageuzi ya
kiuchumi.
Ameponea majaribio kadhaa ya kuuawa ambapo wafuasi wa Mugabe
wanatuhumiwa kuyatekeleza.
Chamisa, kwa upande wake alikuwa mbunge akiwana umri wa miaka
25, huenda akawa kiongozi mwenye umri mdogo nchini.
Amneahidi kuujenga upya uchumi wa taifa hilio ,lakini
ameshutumiwa kwa kutoa ahadi za matumizi ya kupindukia - kama vile kuidhinishwa
kwa treni ya mwendo kasi na kuhakikisha mashndani ya kimataifa ya Olimpiki
yanaandaliwa Zimbabwe.
Lakini mchungaji huyo anaonekana
kupigwa jeki kwa matamshi
aliyotoa rais Mugabe katika
Mugabe, aliyejiuzulu mnamo Novemba mwaka jana wakati jeshi
lilipochukua udhibiti wa nchi , amekataa kumuunga mkono aliyekuwa mshirika wake
Mnangagwa.
Kwa kujibu kauli hiyo, Mnangagwa amemtuhumu aliyekuwa kiongozi
wake kwa kula njama na upinzani.
"Ni wazi kwa kila mtu kuwa Chamisa amekula njama na Mugabe,
hatuwezi tena kuliamini lengo lake la kuigeuza na kulijenga upya taifa
letu," amesema.
Mugabe pia amekataa pia kwamba alipokuwa rais alipanga kukabidhi
uongozi kwa mkewe, Grace, akieleza kuwa uliwa ni "upuuzi mtupu".
-BBC
No comments:
Post a Comment