| Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Anita Moshi (kulia) akikabidhi tuzo kwa baadhi ya wateja wao katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ikiwa ni kutambua mchango wa wateja wao. |
| Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Anita Moshi (wa kwanza kulia) akikabidhi tuzo kwa baadhi ya wateja wao katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja ikiwa ni kutambua mchango wa wateja wao. |
| Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Anita Moshi (wa nne kulia) akiwaongoza baadhi ya wateja kukata keki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. |
| Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Anita Moshi (wa nne kulia) akiwaongoza baadhi ya wateja kukata keki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. |
| Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Anita Moshi (wa nne kulia) akiwaongoza baadhi ya wateja kukata keki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. |
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania - TTCL, limeanza maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 kwa kuwazawadia zawadi baadhi ya wateja wake wa muda mrefu ikiwa ni kutambua mchango wao kwa huduma wanazozitoa.
Miongoni mwa taasisi zilizobahakika kupata tuzo ni pamoja na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Makao Makuu, pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki ya NMB na wateja wengine mbalimbali binafsi waliojumuika katika hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Ofisi za TTCL, Samora jijini Dar es Salaam.
Akizungumza alipokuwa akikabidhi tuzo hizo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Anita Moshi alisema wiki ya huduma kwa wateja ni alama muhimu katika kalenda ya shirika hilo, kwani inawakumbusha wajibu wa msingi wa kumweka mteja mbele kama kiini cha mafanikio ya taasisi hiyo.
Alisema ni kipindi cha kujitathmini, kusikiliza wateja kwa makini, na kuimarisha uhusiano wa kudumu zao kiujumla, na ndio maana wameamua kutoa zawadi ya kutambua wateja wao wakuu na wa muda mrefu.
"Kaulimbiu ya mwaka huu: “Mission: Possible” imetupa nguvu zaidi: Hakuna lisilowezekana tukiamua, tukibuni, na tukishirikiana. Katika wiki ya huduma kwa wateja, inatukumbusha kuona kila changamoto kama fursa ya kuboresha na kutoa suluhisho la kudumu. Kaulimbiu hii itakuwa dira yetu ya kila siku katika utekelezaji wa majukumu ya Shirika katika kutoa huduma kwa wateja. Tutakuwa wabunifu, wenye bidii, na watumishi wenye maono yanayolenga matokeo," Mkurugenzi huyo wa Huduma za Sheria, TTCL.
Aidha aliongeza kuwa, kupitia Mpango Mkakati wa TTCL, wamejipanga kuhakikisha uboreshaji wa miundombinu ya huduma zao inaboresha pia maisha ya Watanzania, kwa kujikita katika utowaji huduma bunifu, nafuu na zenye ubora wa kimataifa, huku wakiweka ukaribu na wateja katika kila hatua.
"..Tumejipanga vyema kuhakikisha huduma bora, za uhakika na zenye ubora wa kimataifa zinawafikia wateja wetu wote — ndani na nje ya Tanzania — kupitia uwekezaji endelevu katika miundombinu ya kisasa na teknolojia za kisasa za mawasiliano.
| Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Bi. Anita Moshi (wa nne kulia) akizungumza katika hafla ya uzinduzi maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. |
"Tunatambua umuhimu mkubwa wa huduma zetu kwa wateja. Shirika linaendelea kutekeleza mpango wa upanuzi wa miundombinu ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo kueneza Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hadi kufikia wilaya zote za Tanzania," alisisitiza, Bi. Moshi.
Sambamba na hilo alibainisha TTCL, itaendelea kuwekeza katika teknolojia za kisasa, kuboresha mifumo, na kuhakikisha huduma bora zinawafikia Watanzania wote popote walipo, hivyo kuwataka waendelee kutumia Kituo chetu cha Huduma kwa Wateja kinachopatikana saa 24, na mitandao ya kijamii, na maduka yao kupata huduma, ushauri, au taarifa muhimu.
| Afisa Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Adeline Berchimance akizungumza katika hafla hiyo. |

No comments:
Post a Comment