RAIS ATANGAZA MAPUMZIKO OKTOBA 29... - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 24 October 2025

RAIS ATANGAZA MAPUMZIKO OKTOBA 29...

TAARIFA KWA UMMA 

OFISI YA RAIS, IKULU,

KAMA inavyofahamika, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza siku ya Jumatano tarehe 29 Oktoba, 2025 kuwa siku ya kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025. 

Aidha, kwa madhumuni ya kuwawezesha wananchi wenye sifa stahiki wakiwemo watumishi wa umma na wafanyakazi katika sekta binafsi kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutumia mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Sikukuu za Kitaifa Sura 35, ameidhinisha tarehe 29 Oktoba, 2025 kuwa siku ya mapumziko.

 Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, os Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka KATIBU MKUU KIONGOZI 24 Oktoba, 2025.

No comments:

Post a Comment