WANANCHI WAMIMINIKA KUPATA ELIMU BANDA LA WIZARA YA FEDHA - SABASABA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 30 June 2025

WANANCHI WAMIMINIKA KUPATA ELIMU BANDA LA WIZARA YA FEDHA - SABASABA

Na Peter Haule, WF, Dar es Salaam
 
WANANCHI wametakiwa kuhakikisha wanakopa katika maeneo rasmi ili kuondoa changamoto ya mikopo umiza ambayo imekuwa ikileta adha kwa wananchi kwa kufilisiwa mali zao.
 
Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) Afisa Mwandamizi wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo amesema Serikali imeweka utaratibu wa kujisajili kwa watoa huduma za fedha ili kukomesha tatizo hilo.
 
Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza tarehe 28 Juni yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu, ambapo Wizara ya Fedha na Taasisi zake zinashiriki kikamilifu kutoa huduma kwa karibu kwa wananchi kupitia Maonesho hayo.

Afisa Mwandamizi wa Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi, Wizara ya Fedha, Bw. Fedrick Sanga, akitoa elimu kuhusu miradi yenye sifa ya kutekelezwa kwa ubia kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu.

Wananchi wakiwa wamejitokeza kupata elimu ya fedha, masuala ya bajeti, sera, pensheni inayolipwa na Hazina na usimamizi wa deni la Taifa, waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Dar Es salaam (Sabasaba) ambayo yameanza  tarehe 28 Juni na kutarajiwa kuhitimishwa Julai 13 mwaka huu. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha).


No comments:

Post a Comment