KAMPUNI ya Bakhresa Group (SSB) ndani ya miaka 50 imefanikiwa kuzalisha kampuni takribani 15 nchini na nyingine nane nje ya nchi huku ikiingiza mapato takribani trilioni 2.68 kwa mwaka ambapo pia ikijivunia kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 10,000 moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 150,000.Hayo yameelezwa leo Juni 17, 2025 Jijini Dar es Salaam wakati Kampuni hiyo ikiadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Suleiman Serera.
Naibu Katibu Mkuu amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi nchini ikiwemo kampuni hiyo katika kukuza uchumi wa Taifa, kuhimiza ajira, na kuendeleza mazingira bora ya biashara nchini.
“Dira yetu ya ukuaji endelevu inategemea ushiriki wa sekta binafsi kwa kiwango kikubwa. Tunazihimiza biashara za ndani kuangalia nje ya mipaka ya taifa na kuchangia kuiweka Tanzania katika nafasi ya ushindani wa kiuchumi kupitia viwanda,” amesema.




No comments:
Post a Comment