![]() |
| Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu kwenye ziara za wadau wa elimu kutembelea shule anuai na kuzungumza na wazazi, viongozi na wadau wengine wa elimu. |
![]() |
| Wanafunzi wakishangilia kwenye moja ya mikutano ya sehemu ya Maadhimisho ya Jumala la Elimu Kitaifa, mkoani Katavi. |
![]() |
| Sehemu ya Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), na wadau wengine wa elimu wakiwa katika moja ya ziara kutembelea shule na kuzungumza na wazazi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho. |
WAZAZI wilayani Mpimbwe Mkoa wa Katavi wametakiwa kutowaficha watoto wenye ulemavu nyumbani na badala yake watoe taarifa kwa viongozi wa vijiji na na shule ili watoto hao waweze kupewa nafasi ya kupata Elimu.
Akizungumza
na Kundi la Wazazi leo katika Kijiji Cha Mbede, wilayani Mpimbwe, wakati wa
Ziara za kutembelea Shule za Maadhimisho ya Juma la Elimu, Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya Maazimisho hayo Kitaifa, Bw. Greyson Mgoi, alisema hakuna
sababu yeyote ya kuwaficha watoto wenye ulemavu nyumbani kwa kuwa nao wanayo
haki ya kupata elimu bora itakayowasaidia katika maisha yao ya badae.
Bw.
Mgoi ambaye pia ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Habari na Uchechemuzi wa Shirika
la Uwezo Tanzania, alisema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatekeleza
Sera ya Elimu bila malipo kwa watoto wote hivyo, si sahihi kwa wazazi wenye
watoto wenye ulemavu kuwaficha ndani.
"Watoto
wenye ulemavu wanayo haki ya kupata Elimu, tusiwanyime haki yao ya msingi, kama
unaye mtoto mwenye ulemavu toa taarifa kwa viongozi katika eneo lako au fika
shuleni itoe taarifa kwa mwalimu mkuu, utaweza kumsaidia mtoto huyo kupata elimu.
Serikali
pamoja na wadau mbalimbali wanafanya jitihada kubwa za kuhakikisha kundi hili
nalo linapata elimu bora," alisema Bw. Mgoi.
Sambamba
na hilo, Mgoi alisema kuwa Wazazi wanapaswa kuwasaidia watoto wote kukuza stadi
za ujuzi mbalimbali suala ambalo ni muhimu kwa maisha yao.
Kauli mbinu ya mwaka huu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu ni Elimu na Ujuzi kwa Maendelea ya Taifa, ambayo inapaswa kutekelezwa kwa vitendo na wadau wote wakiwemo Wazazi ili kuboresha Elimu ya wototo wote.
Maadhimisho ya Juma la Elimu yalizinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mh. Mwanamvua Mrindoko Mei 5, 2025 Katika Kata ya Majimoto, Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi na yanatarajiwa kuhitimishwa Mei 9, 2025.
Wadau
kutoka katika zaidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali 50 yanashiriki kwenye
maadhimisho hayo ya Kitaifa, likiwemo Shirika la Uwezo Tanzania.









No comments:
Post a Comment