RAIS DKT. SAMIA AMKARIBISHA RAIS WA NAMIBIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 20 May 2025

RAIS DKT. SAMIA AMKARIBISHA RAIS WA NAMIBIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kufuatia ziara ya mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah tarehe 20 Mei, 2025. 

Rais wa Jamhuri ya Namibia Mhe. Netumbo Nandi-Ndaitwah akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam kufuatia ziara yake nchini Tanzania tarehe 20 Mei, 2025. 

Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akisalimiana na Bi. Salama Salehe Ghulum (Mama Salehe) ambaye alikuwa jirani yake wakati akiishi Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam katika miaka ya 1980s. Mhe. Rais Dkt. Nandi-Ndaitwah alikutana na jirani yake huyo wa siku nyingi katika hafla ya chakula cha jioni alichoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Namibia Mhe. Dkt. Netumbo Nandi-Ndaitwah akutana na majirani zake alioishi nao Magomeni Mikumi Jijini Dar es Salaam katika miaka ya 1980.

No comments:

Post a Comment