WAZIRI KOMBO AWASILI ANTALYA KWA ZIARA YA KIKAZI - THE HABARII
.com/img/a/
ASAS GROUP
.com/img/a/

Friday, 11 April 2025

demo-image

WAZIRI KOMBO AWASILI ANTALYA KWA ZIARA YA KIKAZI

 

02
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) akiwasili katika uwanja wa ndege wa Antalya.

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amewasili jijini Antalya, Uturiki kwa ziara ya kikazi anayotarajia kuifanya nchini humo kuanzia Aprili 11 hadi 13, 2025. 

 

Akiwa katika ziara hiyo Waziri Kombo atashiriki katika matukio mbalimbali ikiwemo; kushiriki Mkutano wa 4 wa Diplomasia wa Antalya (The Antalya Diplomacy Forum – ADF2025) unaotarajiwa kufanyika Aprili 11 hadi 12, 2025, kufanya mazungumzo ya uwili na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa Serikali na Mashirika ya Kimataifa, na kutia saini Hati ya Makubaliano (MOU) kuhusu uanzishwaji wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) baina ya Tanzania na Uturuki. 

 

Ziara hiyo iliyobeba dhima ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi pamoja na masuala mengine inalenga kuongeza wigo wa fursa za kiuchumi na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na jumuiya ya kimataifa huku ikitilia mkazo zaidi katika sekta ya biashara na uwekezaji, afya, elimu, ulinzi na usalama na Utalii. 

 

Aidha, ushiriki wa Tanzania kwa mara ya kwanza katika mkutano wa ADF2025 tokea kuanzishwa kwake, kunashiria azma ya serikali ya kutumia ushawishi wake wa kidiplomasia katika kutafuta fursa, kulinda na kutetea maslahi ya Tanzania kwa manufaa ya wananchi wake kupita majukwa mbalimbali ya kimataifa.

 

Mkutano wa ADF2025 utawakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali, Mawaziri wa Mambo ya Nje, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, manguli wadiplomasia, watunga sera, wafanyabiashara, wanataaluma, na wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka kote duniani kwa lengo la kujadili na kutafuta majawabu ya changamoto mbalimbali zinazo ikabili dunia ikiwemo amani na usalama, uchumi na siasa.

 

Miongoni mwa viongozi atakaofanya nao mazungumzo pembezoni mwa mkutano wa ADF2025 ni pamoja na; Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mhe. Hakan Fidan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Mhe. Andrii Sybiha, Waziri wa Fedha wa Uturuki Mhe. Mehmet Simsek, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Teknolojia ya Umoja Mataifa kwa Nchi zinazoendelea Bw. Deodat Maharaj, Rais wa Jamhuri ya Kosovo Mhe. Vjosa Osmani-Sadriu na Rais wa Taasisi ya Turkish Maarif Foundation. 


Halotel+Mpango+Mzima

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *