CCM YAMCHAGUA DK. SAMIA KUGOMBEA URAIS, DK. NCHIMBI MGOMBEA MWENZA…! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Sunday, 19 January 2025

CCM YAMCHAGUA DK. SAMIA KUGOMBEA URAIS, DK. NCHIMBI MGOMBEA MWENZA…!

Shamrashamra za Wajumbe pamoja na wageni mbalimbali ndani ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma mara baada ya kutangazwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais katika Uchaguzi utakaofanyika badae mwaka huu. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan amechaguliwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho kuwa Mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka huu. Katika mkutano huo Rais Dkt. Samia alipata kura za ndio 1924 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa. 

Wajumbe wa NEC, CCM wamepitisha jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upande Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kugombea nafasi ya Urais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Dk. Samia) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (Dk. Mwinyi) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Dk. Samia akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM pamoja na wageni mbalimbali wakati akifunga mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete tarehe 19 Januari, 2025.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025.

Dk Nchimbi ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar. 

Dk. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.

Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi, ambaye atakuwa mgombea mwenza mchaguzi mkuu wa mwaka huu kupitia CCM.

No comments:

Post a Comment