Na Dotto
Mwaibale, Dar es Salaam
WATOTO
Mapacha ambao mama yao amepata changamoto ya maradhi ya moyo muda mfupi tangu alipojifungua
wakazi wa Kongowe Kibaha mkoani Pwani wanahitaji msaada wa hali na mali wa
matunzo.
Mama ya
watoto hao Amina Mohamed Simba (28) ambaye baada ya kupata changamoto hiyo
alipelekwa Hosptali ya Tumbi Kibaha lakini kufuatia hali yake kuwa mbaya
amehamishiwa Hospitali ya Mlongazila jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi
ambapo inaelezwa kuwa bado hali yake sio nzuri.
Watoto hao
hivi sasa wanalelewa na bibi yao ambaye hana uwezo ambapo wanaiomba jamii
kujitokeza kusaidia malezi ya watoto hao kutokana na kutegemea maziwa ya kopo tu.
Katibu wa
Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Kongowe Kibaha, Saidi
Kibaya akizungumza na mwandishi wa habari hii alisema watoto hao wa miezi
miwili wanalelelewa na bibi yao mzaa mama yao ambaye hana uwezo na kuwa
wanaomba msaada huo kutokana na mahitaji yao hasa kwa upande wa chakula kuwa makubwa
ndio maana wameona jambo hilo kulieleza kwa jamii kwa ajili ya kuongeza nguvu
ya kuwasaidia watoto hao malaika wa Mungu.
“Mama ya
watoto hawa ni mkazi wa Kongowe Kibaha alipojifungua tu alipatwa na
changamoto ya maradhi ya moyo na kupoteza fahamu tangu hapo hali yake sio nzuri
alikuwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) Hospitali ya Tumbi lakini hivi sasa
amehamishiwa Hospitali ya Mlongazila kwa ajili ya matibabu zaidi,” alisema Kibaya.
“Leo mimi na
viongozi wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la
Kongowe akiwepo Mwenyekiti wa chama hicho tulikwenda kuwaona watoto hao ambapo
tuliambiwa kuna mdau mmoja waliye mtaja kwa jina moja la Mwamwaja ambaye
aliguswa na changamoto ya watoto hao
alitoa Sh.150,000 ili zitumike kuwanunulia maziwa,” alisema Kibaya.
Kibaya
aliiomba jamii na Serikali kuwasaidia watoto hao ili waweze kupata chakula
pamoja na bibi yao huyo ambaye hana uwezo wowote.
Ndugu
Mtanzania watoto hawa kulwa na Dotto ni watoto wetu wanahitaji msaada wako wa
mali na hali kwani kutoa ni moyo na wala sio utajiri.
Aliyeguswa kuwasaidia watoto hao kwa kiasi chochote cha fedha anaweza kuwasiliana na mwandishi wa taarifa hii kwa namba 0754-362990 au kwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Tawi la Kongowe, Saidi Kibaya kwa namba ya simu 0655-075310. Kazi iendelee.
No comments:
Post a Comment