RAIS DKT. SAMIA AWASILI NCHINI BRAZIL, KUSHIRIKI MKUTANO WA G20 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya

Sunday, 17 November 2024

RAIS DKT. SAMIA AWASILI NCHINI BRAZIL, KUSHIRIKI MKUTANO WA G20

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya ua kutoka kwa mtoto Joanna Mghamba mara baada ya kuwasili Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil tarehe 16 Novemba, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Galeão Air Force Base Jijini Rio de Janeiro nchini Brazil tarehe 16 Novemba, 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Kundi la G20.  Rais Dkt. Samia amealikwa na Rais wa Brazil Mhe. Luiz Inácio Lula da Silva ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki mijadala inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa na umaskini, kuchochea maendeleo endelevu na matumizi ya nishati mbadala.

No comments:

Post a Comment