MHE. PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA SERIKALI YA BOTSWANA JIJINI GABORONE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 22 October 2024

MHE. PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA SERIKALI YA BOTSWANA JIJINI GABORONE

MKUU wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-SEOM) Mhe. Mizengo Pinda, amekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Kabo Morwaeng na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana Mhe. Dkt. Lemongang Kwape alipotembelea Ofisi ya Rais wa Botswana jijini Gaborone. 

Mhe. Pinda amekutana na viongozi hao kwa lengo la kujitambulisha kama Mkuu wa Misheni ya SADC na kuwatambulisha wajumbe wa misheni hiyo ambao wako nchini Botswana kwa ajili ya Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika tarehe 30 Oktoba, 2024. 

Mhe.Pinda aliambatana na Sekretarieti ya SADC, wajumbe wa SADC Organ TROIKA, Baraza la Ushauri wa Uchaguzi la SADC, na Waangalizi wa SADC. Mhe. Pinda aliwaambia wenyeji wake kwamba SEOM ipo Botswana tayari kwa kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi. 

Mhe. Pinda aliisifu Botswana kwa maendeleo makubwa ya kiuchumi pamoja na amani na us

No comments:

Post a Comment