KITUO CHA NNE CHA KUJAZA MAGARI KUANZA KAZI BAADA YA SIKU 90 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday 25 October 2024

KITUO CHA NNE CHA KUJAZA MAGARI KUANZA KAZI BAADA YA SIKU 90

 



KAMPUNI ya TAQA-Dalbit Tanzania Ltd imetiliana saini mkataba na kampuni ya BQ contractors Ltd kwa ajili ya ujenzi wa uunganishaji wa bomba la gesi asilia kutoka TPDC lenye kipenyo cha nchi 12 Bomba linaloenda kunganishwa na bomba linalopita barabara ya Sam Nujoma eneo la Mlimani City ambapo panaenda kujengwa kituo cha cha Dalbit CNG. 

Kuunganishwa kwa bomba hili kutakapokamilika itakuwa hatua nyingine ya kuongeza kituo cha nne cha kujaza Gesi Asilia CNG na wadau binafsi katika Jiji la Dar es Salaam.

Muda wa mkataba huu wa Uhandisi, Ununuzi na Ujenzi (EPC) ni siku 90 na utajumuisha usambazaji wa mabomba ya usambazaji wa gesi asilia, Kituo cha Kupunguza Shinikizo kutoka nje (PRS) na viunga vya mabomba.

Zoezi la utiliaji saini mkataba huo ukifanyika na Mkurugenzi Mkuu wa TAQA Dalbit Bw. Amr Aboushady akiwa na mwenzake Eng. Prof John Bura, Mkurugenzi Mtendaji wa BQ Contractors Ltd. Ukshuhudiwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa BQ Bw. Silas John Bura na Bw. Habibu Halifa wa TAQA - Dalbit Tanzania Ltd.

#TanzaniaEnergy #NaturalGasPipeline #SustainableFuture #EnergyInfrastructure #BQContractors #TaqaDalbit #NaturalGas

No comments:

Post a Comment