Adeladius Makwega-MWANZA
Umoja wa Wanafuzi Wakatoliki
wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu Tanzania(TMCS) umewataka wanachama wake kuhakikisha
wanatoa michango yao kwa wakati na kwa kufanya hivyo watasaidia umoja wao
kutimza majukumu yake ya kila siku na wanachama watakuwa wametimiza wajibu wao
kwa chama na kwa Mungu.
Hayo yamesemwa katika viunga vya Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya na Mtunza Fedha
wa umoja huo Kanda ya Mwanza Bi. Merina Pascal wakati akizungumza na wanachama
wa tawi la chuo hiki alipotembelea kufuatilia maendeleo ya uhai wa tawi hilo.
“Tupo hapa kwenu,
tunawakumbusha kutoa michango yote kama ilivyo ili kusaidia viongozi wenu
kupata moyo wa majukumu haya ya kiimani ili waweze kuwaongoza vema.”
Katika ziara hiyo Bi. Merina
Pascal aliambatana na Mhazini Msaidizi TMCS Jimbo ndugu Robert Mlay na miongoni
mwa majukumu waliyofanya ni kusimamia uchaguzi wa viongozi wa tawi hilo.
Katika uchaguzi huo viongozi
kadhaa walichaguliwa;
“Abrahamu Engidongi Rundo
(Mwenyekiti) Francis Lukas Maramonyi (Makamu Mwenyekiti)
Alphonce Sadock (Katibu)
Mariamu Kabanya
Seleli(Katibu Msaidizi)
Francis Joachim Panga(Mhasibu)
Akizungumza mara baada ya uchaguzi
huo Mwenyekiti wa tawi la TMCS Malya Abrahamu Rundo ameshukuru kwa kuchaguliwa,
akitoa ahadi kuwa hatowaangusha huku akiomba ushirikiano kwa kila mwanachama.
Kwa upande wake Mkufunzi
Mlezi TMCS tawi hilo Denis Kayombo alisema kuwa anawapongeza wanachama wote
waliochaguliwa kwa nafasi zote na anawapongeza pia wale waliopiga kura,
“Kikubwa
kwenu tambueni kuwa TMCS pia ni pahala pakujifunza uongozi, mvumiliane kila
mmoja na madhaifu yake, viongozi ni binadamu na hata wapiga kura ni binadamu
pia. Uongozi wa dini siyo wa kuukwepa kesho unaweza kusimama sehemu ukasema ‘Jamani
mimi nilikuwa kiongozi TMCS pale Malya.’ Hilo likafanya wewe uaminike, fanyeni
kazi kwa bidii na moyo wote.”
TMCS ni Umoja wa Wanafunzi
Wakatoliki wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu Tanzania ambapo ulianzishwa mwaka
1984 pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo wazo hilo likakuzwa zaidi mwaka
2006 kwa kuhusisha vyuo kadhaa na mwaka 2009 wakichaguliwa viongozi wa umoja
huo.
TMCS inatokana na Umoja wa
Wanafunzi Wakatoliki Ulimwenguni (IMCS) ambao ulianzishwa mwaka 1921 huko
Fribourg Uswiswi.


No comments:
Post a Comment