Jamii
imeaswa kuwatembelea Watoto wanaolelewa katika Makao ya Kulelea Watoto ili
kuwajenga kisaikolojia kwa kuwa wengi wa Watoto hao wanatoka katika mazingira
yenye historia ngumu.
Wito
huo umetolewa na Jonas Tarimo, Meneja wa Makao ya Taifa ya Kulelea Watoto
Kikombo jijini Dodoma, alipokuwa akitoa taarifa kuhusu shughuli za Makao hayo
kwa Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa waliyofika kutoa mkono wa
Sikukuu mwishoni mwa wiki.
“Watoto
hawa wanatoka katika uzoefu mgumu, ndoa zenye migogoro, unyanyasaji na wengine
hawana familia kabisa, hivyo mnapofika hivi wakaona sura mpya, mkaongea nao,
mnatusaidia sana kuwajenga kisaikolojia” Alisema Tarimo.
Aidha,
Tarimo alisisitiza kuwa, msaada ni muhimu ingawa kufika katika vituo hivyo ni
muhimu zaidi kwa kuwa ni Watoto wa jamii, kuongea nao hupanua mawanda ya uelewa
wao na kuwapa mtazamo mpya wa maisha.
Dkt.
George Dilunga, Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Mkuu wa Idara ya Magonjwa hayo
BMH, anasema kuwa hatua ya kutembelea Makao ya Kitaifa Kikombo inafuatia
uhusiano uliyopo baina ya taaisi hizo mbili.
“tumekuwa
tukitoa huduma za Afya kwa Watoto wanaoishi hapa kwa kuwafanyia uchunguzi na
matibabu kila baada ya miezi mitatu tangu Juni 16, 2021 yalipozinduliwa Makao
haya hivyo wamekuwa sehemu ya familia yetu” alisema Dkt. Dilunga.
Dkt.
Dilunga aliongeza kuwa, uamuzi wa kujumuika nao msimu huu wa Sikukuu, ulilenga
kuongea na Watoto hao kama sehemu ya kuwapa faraja msimu huu wa sikukuu.
BMH
ilikabidhi Nguo, Jora la kushona sare za shule, seti maalumu kukidhi mahitaji
ya shule iliyohusisha Daftari, Kalamu na Rula kwa Watoto zaidi ya 80 ambayo ni
michango ya wafanyakazi wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa BMH.
Ifahamike
kuwa, kuna zaidi ya Watoto 24,000 wanaolelewa katika makao zaidi ya 320
yaliyosajiliwa katika sehemu mbalimbali nchini, Watoto hao ni zao la migogoro
ya ndoa, unyanyasaji, vifo vya wazazi, Watoto kutelekezwa miongoni mwa sababu
nyinginezo.

No comments:
Post a Comment