Naibu Waziri wa
Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile katika picha ya pamoja na Wakandarasi wa Kampuni
ya LOCA Muhendislik Gemi Mak. PLas Ve Gd. San Tic ltd Sti ya nchini Uturuki na
sehemu ya Vongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya hafla ya utiaji saini
mkataba wa mradi wa ujenzi wa boti yenye vifaa vya matibabu (Ambulance Boat),
iliyofanyika jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa
Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana
Bi. Amina Makilagi wakati wa wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi
wa ujenzi wa boti yenye vifaa vya matibabu (Ambulance Boat), iliyofanyika
jijini Mwanza.
Akizungumza
wakati wa utiaji saini mkataba huo baina ya TASAC na Kampuni ya LOCA
Muhendislik Gemi Mak. PLas Ve Gd. San Tic ltd Sti ya nchini Uturuki jijini
Mwanza Naibu Waziri Kihenzile amesema kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha
utoaji wa huduma za matibabu kwa wananchi na watumiaji wa usafiri majini
hususani nyakati za majanga.
“Serikali
inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri kwa wananchi
wanaotumia Ziwa Viktoria na kupitia mradi huu sasa wa boti yenye vifaa tiba
kutaokoa watumiaji wa usafiiri wa majini na wananchi kwa ujumla kwa kupata
huduma za afya pindi inapotokea ajali katika ziwa viktoria”amesema Naibu Waziri
Kihenzile.
Naibu
Waziri Kihenzile ameongeza kuwa pamoja na utekelezaji wa mradi huo kwa sasa
Serikali iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi wa ya ujenzi wa
kituo cha Utafutaji na Ukoaji ambacho kitafanya kazi kwa ushirikiano na kituo
cha Dar es Salaam ili kuimarisha usalama katika usafiri majini.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bi. Amina Makilagi ameishukuru Serikali kwa
kuendelea kuimarisha usafiri huo kwa kuwekeza katika ujenzi wa meli na
maboresho ya miundombinu lengo likiwa kuchagiza uchukuzi katika Ziwa Viktoria.
Mkuu
wa Wilaya Makilagi ameongeza kuwa mradi huu umekuja wakati muafaka kwani
kukamilika kwake kutachangia kuokoa maisha ya wananchi kwani watapata huduma
hiyo kwa wakati.
Naye
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Musa Mandia amemuhakikishia Naibu Waziri
Kihenzile kuwa Bodi na Menejimneti zimejipanga kuhakikisha mradi huo
unakamilika kwa wakati na viwango.

No comments:
Post a Comment