MBARAWA AITAKA BODI YA TAA KUWA NA VYANZO VINGI VYA MAPATO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 4 October 2023

MBARAWA AITAKA BODI YA TAA KUWA NA VYANZO VINGI VYA MAPATO

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na Wajumbe wa Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) hawapo pichani, wakati alipozindua bodi ya TAA jijini Dodoma leo.

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akimkabidhi vitendea kazi mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA)  Mhandisi  Baraka Mwambage mara baada ya kuzindua bodi hiyo hawapo,  jijini Dare es Salaam leo.

WAZIRI wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameitaka Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA) kuhakikisha TAA inakuwa na vyanzo vingi vya Mapato ili kutoa huduma nzuri zaidi.


Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati alipozindua rasmi bodi hiyo Waziri Prof. Mbarawa amesema uwepo wa vyanzo nje ya vile vinavyotozwa kupitia huduma za uendeshaji utaiwezesha TAA kuboresha viwanja vingi zaidi kwa muda mfupi.


“Kuna mapato mengi sana ambayo yanapatikana nje ya huduma za moja kwa moja zinazotolewa ndani ya Kiwanja, mkiweza kuja na mpango madhubuti kwenye eneo hilo TAA itafika mbali na itatimiza malengo yake kwa wakati’ amesema Waziri Mbarawa.


Waziri Prof. Mbarawa ameitaka TAA kuhakikisha inapelekea watumishi wake kujifunza katika vya ndege mbalimbali duniani ili kuwaongezea ujuzi na utaalaam katika utendaji wa kazi.


Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Juma Fimbo amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa watasimamia maeneo yote ikiwemo mifumo mipya iliyosimikwa viwanjani ili kutoa huduma za kisasa na viwango.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utalawa na Rasilimali Watu Lucas Kambelenje maewapongeza wajumbe wa bodi hiyo kwa kuteuliwa na kuwasisitiza kuzingatia miongozo.


Bodi ya TAA iiliyozinduliwa inajumuisha wajumbe inaongozwa na Mwenyekiti Juma Fimbo, Mhandisi Baraka Mwambage, Meshack Anyingisye, John Njawa, Plasduce Mbosa na Biseko Chiganga.

(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Uchukuzi)

No comments:

Post a Comment