MABORESHO YA BANDAI KUSHIRIKISHA WADAU - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday 20 July 2023

MABORESHO YA BANDAI KUSHIRIKISHA WADAU

Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Aron Kisaka akisisitiza jambo kwa wadau huduma za Bandari Nchini (hawapo pichani) wakati alipofungua mkutano wa kamati hiyo kwa bandari za Ziwa Tanganyika, uliofanyika Kigoma Mkoani humo.

SERIKALI imesema itaendelea kuhakikisha wadau wote wanashirikiswa katika hatua mbalimbali za maboresho ya bandari nchini ili kurahisisha shughuli za uchukuzi na kuongeza ufanisi wa bandari hizo.  

Akizungumza mjini Kigoma wakati akifungua Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Maboresho ya Huduma za Bandari kwa bandari za Ziwa Tanganyika, Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Mhandisi Aron Kisaka amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha mizigo yote ya ndani na nje ya nchi hususani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inahudumia kupitia bandari ka Kigoma ili kurahisisha biashara.

“DRC pekee yake inatumia bandari ya Kigoma kwa kusafirisha zaidi ya tani elfu kumi sasa kwa maboresho tuliyoyafanya ndani ya kipindi hiki kifupi ni lazima tuhakikishe idadi ya mzigo unaohudumiwa unaongezeka ili thamani ya fedha iliyowekezwa ionekane’ amesema Mhandisi Kisaka.

Mhandisi Kisaka amesema pamoja na maboresho yanayoendelea kufanyika ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari TPA kuhakikisha idara ya masoko inajipanga kutafuta mzigo kwa ajili ya bandari kubwa ya Karema ili kuifanya bandari hiyo kuwa na ufanisi baada ya ujenzi wake kukamilika. 

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Bw. Edward Mabula  amesema zaidi ya shilingi bilioni 100 zimetumika kufanya maboresho ya miundombinu na vifaa katika bandari za Ziwa hilo ikiwemo bandari ya Kigoma, Kibirizi, Ujiji na Karema.

Bw. Mabula ameongeza kuwa kwa sasa TPA imeingia makubaliano na Serikali ya DRC kwa ajili ya kujenga bandari kavu eneo la Kalemi na Kasumbalesa ambapo hatua hiyo itaongeza usafirishaji wa shehena ya mizigo hadi kufikia tani laki 330.

Naye Mdau wa Bandari nchini na Mkurugenzi Mtendaji wa Malagarasi Shipping Company Bw. Mbarak Hamoud ameishukuru Serikali kwa kuanzisha vikao vya maboresho ya utendaji wa bandari kwani hatua hiyo itaongeza ufanisi na tija kwa kujadili na kutafuta suluhu kwa pamoja kwa hatua zote za maboresho yanayofanyika katika bandari hizo.


No comments:

Post a Comment