Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang'a. |
TAARIFA hii inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa hali ya joto, upepo na mvua katika msimu wa Juni hadi Agosti (JJA), 2023; Ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao. Kwa kawaida, kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti (JJA), hutawaliwa na hali ya baridi na upepo mkali kwa maeneo mengi ya nchi. Kwa muhtasari, mwelekeo wa msimu wa JJA, 2023 unaonesha kuwa:
a) Mwelekeo wa hali ya joto
i. Hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na nyanda za juu kusini-magharibi.
ii. Vipindi vya baridi zaidi vinatarajiwa kujitokeza mwezi Juni.
iii. Vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache ya ukanda wa pwani.
b) Mwelekeo wa hali ya upepo
i. Upepo wa wastani unatarajiwa kushamiri katika maeneo mengi nchini.
c) Athari
i. Magonjwa yanayohusiana na hali ya hewa ya baridi kama vile homa ya mapafu na magonjwa ya mifugo yanaweza kujitokeza, ingawa kwa kiasi kidogo.
ii. Hali ya vumbi linalosababishwa na upepo katika baadhi ya maeneo linaweza kupelekea uwepo wa magonjwa ya macho.
1.0 MATARAJIO YA VIWANGO VYA JOTO KWA MIEZI YA JUNI HADI AGOSTI, 2023
Katika kipindi cha JJA, 2023 hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo ya nyanda za juu kusini -magharibi pamoja na ukanda wa Ziwa Victoria. Aidha, vipindi vya baridi zaidi vinatarajiwa kujitokeza mwezi Juni.
1.1 Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Kagera, Shinyanga na Simiyu):
Hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi. Kiwango cha joto la chini kinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 13 oC na 19 oC.
1.2 Ukanda wa pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba):
Hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi. Kiwango cha joto la chini kinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 22oC na 26oC kwa maeneo ya mwambao wa pwani na visiwani na kati ya nyuzi joto 19oC na 22oC katika maeneo ya nchi kavu. Hata hivyo, maeneno yenye miinuko yanatarajiwa kuwa na kiwango cha nyuzi joto chini ya 19oC.
1.3 Kanda ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara):
Hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi, kiwango hicho kinatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 13 oC na 21 oC. Hata hivyo, maeneno yenye miinuko yanatarajiwa kuwa na kiwango cha nyuzi joto chini ya 13 oC.
1.4 Kanda ya magharibi (Mikoa ya Tabora, Rukwa, Katavi na Kigoma):
Hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi ambapo joto la chini linatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 15 oC na 19 oC.
1.5 Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma):
Hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi ambapo joto linatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 14oC na 19oC.
1.6 Ukanda wa pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi):
Hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi ambapo joto linatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 16 oC na 22 oC.
1.7 Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma):
Hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani inatarajiwa katika maeneo mengi ambapo joto linatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 11oC na 16 oC.
1.8 Kanda ya nyanda za juu kusini-magharibi (Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe pamoja na maeneo ya kusini ya mkoa wa Morogoro):
Hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi inatarajiwa katika maeneo mengi ambapo joto linatarajiwa kuwa kati ya nyuzi joto 7 oC na 16 oC. Hata hivyo, katika maeneo ya miinuko kiwango hicho kinatarajiwa kuwa chini ya nyuzi joto 7 oC.

2.0 MWENENDO WA UPEPO KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI (JJA), 2023
Kwa kawaida msimu wa Kipupwe hutawaliwa na upepo wa Kusi. Hata hivyo, msimu wa JJA, 2023 unatarajiwa kuwa na upepo utakaovuma kutoka kusini-mashariki na mashariki (Matlai) katika ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi na maeneo ya nchi kavu. Kwa ujumla, upepo wa wastani unatarajiwa kushamiri katika maeneo mengi nchini.
3.0 MWELEKEO WA MVUA KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI, 2023
Kwa kawaida kipindi cha JJA kinatawaliwa na hali ya ukavu katika maeneo mengi ya nchi. Hata hivyo, upepo kutoka kusini-mashariki hadi mashariki unatarajiwa kuleta unyevunyevu kutoka katika Bahari ya Hindi ambao unaweza kusababisha vipindi vya mvua katika maeneo machache ya ukanda wa pwani (mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).
4.0 MIFUMO YA HALI YA HEWA
Katika kipindi cha msimu wa Kipupwe (Juni hadi Agosti), 2023, hali ya joto la bahari katika ukanda wa tropiki ya kati ya bahari ya Pasifiki inatarajiwa kuwa ya juu ya wastani, hali inayoashiria uwepo wa El Niño ambayo inatarajiwa kuendelea kuimarika katika kipindi chote cha msimu na hata baada ya msimu. Vilevile, uwepo wa El Niño katika kipindi cha msimu wa JJA 2023, inatarajiwa kusababisha mchango mdogo katika mwenendo wa mvua nchini hususan maeneo ya pwani.
Hali ya joto la bahari la wastani hadi chini ya wastani inatarajiwa katika eneo la mashariki mwa bahari ya Hindi (Pwani ya Indonesia) na joto la baharí la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la magharibi mwa bahari ya Hindi (pwani ya Afrika Mashariki). Hali hii inatarajiwa kuimarisha mifumo inayosababisha vipindi vya mvua katika maeneo machache ya ukanda wa pwani. Kwa upande mwingine, joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la bahari kusini-mashariki mwa bahari ya Atlantiki (Pwani ya Angola). Hali hii inatarajiwa kusababisha hali ya ukavu hususan katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria, magharibi, nyanda za juu kusini magharibi na maeneo ya kati ya nchi.
Aidha, joto la bahari la juu kidogo ya wastani linatarajiwa katika eneo kubwa la kusini magharibi mwa bahari ya Hindi (kusini mashariki mwa Madagascar). Hali hii inatarajiwa kupunguza nguvu ya mifumo ya mgandamizo mkubwa wa hewa iliyopo katika kizio cha kusini, kasi na uwepo wa vipindi vya upepo wa kusi na hali ya ubaridi kwenye maeneo mengi nchini.
5.0 ATHARI NA USHAURI
Athari na ushauri kwa wadau wa sekta mbalimbali ni kama ifuatavyo:
5.1 Athari
Katika kipindi hiki, magonjwa yanayohusiana na hali ya hewa ya baridi kama vile homa ya mapafu na magonjwa ya mifugo yanaweza kujitokeza, ingawa kwa kiasi kidogo. Pia, vumbi linalosababishwa na upepo katika baadhi ya maeneo linaweza kupelekea uwepo wa magonjwa ya macho na mengine yanayohusiana na hali hiyo.
5.2 Ushauri
Tahadhari za kiafya zichukuliwe ili kulinda jamii dhidi ya magonjwa yanayoweza kusababishwa na baridi, vumbi na matumizi ya maji yasiyo safi na salama. Kutokana na hali ya ukavu inayotarajiwa katika maeneo mengi katika kipindi hiki, maji na malisho yanapaswa kutumika kwa uangalifu ili kupunguza athari zinazotarajiwa. Wafugaji kuendelea kuzingatia ratiba za kuogesha mifugo ili kudhibiti magonjwa ya mifugo na kufuata ushauri wa wataalam. Aidha, wakulima wanapaswa kuhamasishwa kulima mbogamboga na mazao ya mizizi kama vile viazi katika maeneo oevu na pia katika maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya mvua katika kipindi hiki. Sekta za ujenzi, madini na uchukuzi zinaweza kunufaika kutokana na hali ya hewa inayotarajiwa.
Angalizo:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) itaendelea kufuatilia mifumo ya hali ya hewa na kutoa mrejesho. Watumiaji wa taarifa za utabiri huu wanashauriwa pia kufuatilia na kuzingatia utabiri wa saa 24, siku 10, mwezi pamoja na tahadhari za hali mbaya ya hewa kama zinavyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Imetolewa: 26 Mei, 2023
Na: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
No comments:
Post a Comment