SERIKALI NA WAFANYABIASHARA KARIAKOO WAKUBALIANA....! - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 15 May 2023

SERIKALI NA WAFANYABIASHARA KARIAKOO WAKUBALIANA....!


- Wasitisha Mgomo wa kufunga maduka

KUFUATIA wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo kupanga kufanya Mgomo wa kufunga maduka kushinikiza Serikali kutatua kero zao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla mapema leo amekutana na wafanyabiashara hao na kufanikiwa kumaliza Mgomo huo.

Akitoa tamko la Serikali, CPA, Makalla amesema Serikali imewaelekeza TRA kusitisha Operesheni ya Kamatakamata mpaka pale ufumbuzi wa pamoja utakapopatikana.

Aidha CPA, Makalla amesema ifikapo Alhamis ya May 18 Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa atafanya kikao na Kamati ya Wafanyabiashara wa Kariakoo Saa 5 asubuh ofisi ya Waziri mkuu Magogoni DSM Ili kupata Suluhu ya pamoja kumaliza tatizo hilo ambapo kwenye kikao hicho kitajumuisha pia mawaziri wa kisekta.

Pamoja na hayo CPA, Makalla ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kuendelea kufanya biashara kwa amani na Utulivu wakati Serikali ikiendelea kufanyia kazi madai Yao huku akihimiza kulipa Kodi kwa mujibu wa Sheria.

Baada kukamilika kwa kikao hicho Cha maridhiano, Wafanyabiashara wote walielekea kwenye maduka Yao na kuyafungua ambapo baadhi ya Wafanyabiashara wamemshukuru Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza na kutatua kero Yao kwa wakati na wameahidi kushirikiana na Serikali.

No comments:

Post a Comment