RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA KITAALUMA WA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA (TAPSEA) PAMOJA NA MENEJIMENTI YA WATUNZA KUMBUKUMBU NA NYARAKA (TRAMPA), ZANZIBAR - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 27 May 2023

RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA KITAALUMA WA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA (TAPSEA) PAMOJA NA MENEJIMENTI YA WATUNZA KUMBUKUMBU NA NYARAKA (TRAMPA), ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi, Makatibu Mahsusi pamoja na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka kabla ya kufunga Mkutano wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye viwanja vya Fumba kwa ajili ya kushiriki Kikao maalum cha Makatibu Mahsusi pamoja na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka kabla ya kufunga Mkutano wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika katika Viwanja vya Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023.


Baadhi ya Viongozi, Makatibu Mahsusi Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia katika Mkutano wao uliofanyika Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023.

Shamrashamra za Makatibu Mahsusi pamoja na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa kilele cha Mkutano wao wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023.

Viongozi wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) wakila Kiapo cha Kutunza Siri pamoja na Makatibu Mahsusi, Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa kilele cha Mkutano wao wa Kitaaluma uliofanyika Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Hati ya Kiwanja Mwenyekiti wa Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) Devota George Mrope mara baada ya kufunga mkutano Maalum wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Pongezi na Shukrani kutoka (TAPSEA) na (TRAMPA) iliyokabidhiwa kwake na  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa mkutano wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) kilichofanyika Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye viwanja vya Fumba kwa ajili ya kushiriki Kikao maalum cha Makatibu Mahsusi pamoja na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka kabla ya kufunga Mkutano wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika katika Viwanja vya Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023.

No comments:

Post a Comment