TMA YAWANOA WANAHABARI KUHUSU MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA 2023 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 21 February 2023

TMA YAWANOA WANAHABARI KUHUSU MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA 2023

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang'a akizungumza kwenye warsha hiyo iliyofanyika Mjini Kibaha.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang'a (kulia) akisisitiza jambo kwa washiriki wa warsha hiyo iliyofanyika Mjini Kibaha.

Warsha ikiendelea.

Warsha hiyo iliyofanyika Mjini Kibaha ikiendelea.

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesisitiza umuhimu wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kutolewa kwa uhakika, usahihi na kwa wakati kwa ajili ya maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi. Haya yalizingumzwa na Kaimu Mkurugunzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Ladislaus Chang’a wakati akifungua Warsha ya wanahabari inayohusu mwelekeo wa msimu wa mvua za Masika kwa kipindi cha mwezi machi hadi mei 2023 yenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kwa maendeleo endelevu”.

“Kama mnavyofahamu warsha hii ni muendelezo wa juhudi za kuhakikisha taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa kwa uhakika, usahihi na kwa wakati. Napenda kuendelea kuwashukuru wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii (Online Media) kwa kuendelea kuwa nguzo muhimu katika kusambaza na kufikisha taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa watumiaji yaani jamii kwa ujumla Hii imesaidia katika kuongeza uelewa na mwamko wa jamii katika kufuatilia na kutumia taarifa za hali ya hewa” Alisema Dkt Chang’a.

Kwa kusisitiza, Dr Chang’a Alisema ” Kuongezeka kwa mwamko na uelewa kuhusu taarifa za hali ya hewa ni muhimu kwa taarifa hizi zikiifikia jamii kwa wakati, uhakika na usahihi itaisaidia jamii kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa. Vilevile, taarifa mahsusi za hali ya hewa kwaajili ya matumizi ya sekta mbalimbali zinasaidia katika ukuaji wa kiuchumi. Pia itazisaidia mamlaka zinazohusika kupanga mipango ya kukabiliana na majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa, mikakati ya kimaendeleo, upatikanaji wa chakula na lishe bora pamoja na afya kwa ustawi wa jamii kwa ujumla.”

Wanahabari nao walitoa pongezi na shukurani kwa Mamlaka ya hali ya hewa kwa ushirikiano wanaoendelea kupata katika uwasilishwaji wa taarifa za hali ya hewa kwa Jamii. Ushirikiano huu unatolewa kwa njia za Mafunzo ya wanahabari hapa nchini na nje ya nchi. Haya yalisemwa na Ndg Dorcas Raymos wa Channel 10, Akiwasilisha Taarifa la Jopo la wanahabari walioenda nchini kenya kwa mafunzo ya Utolewaji wa taarifa za hali ya hewa.

”Tunaishukuru Mamlaka ya hali ya hewa kwa kutupa fursa ya kushiriki mafunzo yaliyotolewa na ICPAC nchini Kenya. Pamoja na mambo mengine tulinufaika kwa kujifunza mifumo ya ufuatiliaji athari ziletwazo na hali ya mbaya ya hewa (Hazards Watch/ Drought Watch). Mfumo huu utatusaidia kupata taarifa mapema na kuwahabarisha jamiii ili iweze kuchukua tahadhari dhidi ya athari zitokanazo na hali mbaya ya hewa” Alisema Ndg Dorcas Raymos

Kwenye Warsha Hii iliyofanyika Kibaha,Pwani, Wanahabari walipata fursa ya kujua vitu mbalimbali kama Tathmini ya Mvua za ksimu wa vuli (Oktoba hadi disemba 2022), Mwenendo wa Mvua za msiumu wa (Novemba 2022 hadi Aprili 2023). Wanahabari pia walijifunza Lugha na Maneno yanayotumiwa katika uwasilishwaji wa taarifa za utabiri wa Hali ya hewa. Mafunzo haya yalitolewa na wataalam kutoka TMA.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatarajia kutoa Rasmi taarifa ya msimu wa mvua za Masika Tarehe 23 Februabri 2023

No comments:

Post a Comment