KIWANJA CHA NDEGE IRINGA KUKAMILIKA AGOSTI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 15 February 2023

KIWANJA CHA NDEGE IRINGA KUKAMILIKA AGOSTI

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Iringa Mhandisi Daniel Kindole, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Nduli Mkoani Iringa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi. Halima Dendego wakati alipomtembelea ofisini kwake na kujadili hali ya miudombinu Mkoani Iringa.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya Jengo la Zimamoto katika kiwanja cha Ndege cha Nduli Mkoani Iringa. Upanuzi wa Kiwanja hicho unaohusisha Barabara ya Kuruka na Kutua Ndege, barabara ya mchepuo, barabara za usalama, Jengo la Zimamoto na eneo la kuegesha ndege unatajiwa kukamilika katikati ya mwaka 2023. PICHA NA WUU.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya jengo la Zimamoto katika kiwanja cha Ndege cha Nduli Mkoani Iringa. Upanuzi wa Kiwanja hicho unaohusisha Barabara ya Kuruka na Kutua Ndege, barabara ya mchepuo, barabara za usalama, Jengo la Zimamoto na eneo la kuegesha ndege unatajiwa kukamilika katikati ya mwaka 2023. PICHA NA WUU.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya barabara ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 2100 katika Kiwanja cha Ndege cha Nduli Mkoani Iringa.

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya barabara ya kuruka na kutua ndege yenye urefu wa mita 2100 katika Kiwanja cha Ndege cha Nduli Mkoani Iringa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa akimsikiliza Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Iringa Mhandisi Daniel Kindole, kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Nduli Mkoani Iringa.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza Mbunge wa Ismani Mhe. Willium Lukuvi wakati Waziri huyo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Nduli Mkoani Iringa. (Kushoto), ni Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Iringa Mhandisi Daniel Kindole.

WAZIRI  wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema upanuzi na uboreshaji wa miundombinu ya kiwanja cha ndege cha Iringa utakamilika ifikapo Agosti mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa kiwanja hicho mjini Iringa Profesa Mbarawa amesema kiasi cha shilingi bilioni 63.7 kilichotengwa kitakamilisha ujenzi huo na kuondoa kero ya muda mrefu kwa wakazi wa mkoa wa Iringa katika kupata huduma za uhakika za ndege.

“Hadi sasa tumefika asilimia 45 za ujenzi na sehemu iliyobaki tutaikamilisha ifikapo Agosti mwaka huu,” amesema Waziri Profesa Mbarawa.

Aidha, ameongeza kwa kusema kuwa kuanzia Agosti ndege kubwa zitatua katika kiwanja hicho usiku na mchana na zitakuwa zikibeba abiria wengi hivyo kuwataka wakazi wa mkoa wa huo na Njombe kujipanga kuhudumia wataii wengi wanaokwenda katika mbuga ya Taifa ya Ruaha na hivyo kupata manufaa.

Kwa upande wake Mbunge wa Isimani Mhe. William Lukuvi ameishukuru Serikali kwa namna inavyojenga miundombunu mkoani Iringa na kusisitiza kuwa kiwanja cha ndege cha Iringa kitakuwa ufunguo wa utalii na fursa za ajira mkoani humo.

Naye meneja wa Wakala wa Barabara mkoani Iringa Eng. Daniel Kindole amesema ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa unaenda sambamba na uboreshaji wa barabara ya Mchepuo Km 7, na Serikali imepanga kujenga barabara ya Mafinga- Mgololo (Km 80) kwa kiwango cha lami ili kukuza uchumi wa wananchi katika maeneo ya uzalishaji.

No comments:

Post a Comment