WIZARA YA ELIMU YAUPONGEZA UTAFITI WA STADI ZA MAISHA NA MAADILI KWA VIJANA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 25 January 2023

WIZARA YA ELIMU YAUPONGEZA UTAFITI WA STADI ZA MAISHA NA MAADILI KWA VIJANA

Mkurugenzi wa Ithibati Bw. Patrick Lyana (kulia) kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia alipomwakilisha Kamishna wa Elimu kwenye uzinduzi wa Utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana uliofanywa chini ya Mradi wa ALiVE-Tanzania.

Msimamizi wa Mradi AliVE Tanzania Bara, Bi. Devocha Mlay (kushoto) akiwasilisha Utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana uliofanywa chini ya Mradi wa ALiVE-Tanzania.

Mkurugenzi wa Ithibati Bw. Patrick Lyana (kulia) kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akimpongeza Msimamizi wa Mradi AliVE Tanzania Bara, Bi. Devocha Mlay (kushoto) mara baada ya kuzinduwa Utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana uliofanywa chini ya Mradi wa ALiVE-Tanzania.

Wadau anuai wakiwa kwenye uzinduzi wa Utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana uliofanywa chini ya Mradi wa ALiVE-Tanzania.




Mkurugenzi wa Ithibati Bw. Patrick Lyana (kulia) kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akimpongeza Msimamizi wa Mradi AliVE Tanzania Bara, Bi. Devocha Mlay (kushoto) mara baada ya kuzinduwa Utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana uliofanywa chini ya Mradi wa ALiVE-Tanzania.

Mkurugenzi wa Ithibati Bw. Patrick Lyana (kulia) kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akizungumza kabla ya kuzinduwa Utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana uliofanywa chini ya Mradi wa ALiVE-Tanzania.

Mshauri wa Mradi wa ALiVE Kimataifa, Prof. Ester Care akizungumza kabla ya kuzinduwa Utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana uliofanywa chini ya Mradi wa ALiVE-Tanzania.

Kiongozi Mkuu wa Mradi wa AliVE Tanzania, Bi. Khadija Shariff akizungumza kwenye uzinduzi wa Utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana uliofanywa chini ya Mradi wa ALiVE-Tanzania.

Viongozi mbalimbali wa asasi za kiraia, wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana uliofanywa chini ya Mradi wa ALiVE-Tanzania.

Na Joachim Mushi, Dar 

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepongeza utafiti wa stadi za maisha na maadili kwa vijana uliotolewa na Mradi wa ALiVE-Tanzania kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana nchini Tanzania, hivyo kupendekeza uchapishwe na kusambazwa kwa jamii ili uweze kusomwa kabla ya jamii kujitathmini kwa matokeo hayo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Ithibati kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bw. Patrick Lyana alipomwakilisha Kamishna wa Elimu kwenye uzinduzi wa utafiti uliofanyia Tanzania Bara kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana chini ya Mradi wa ALiVE - Tanzania. Kiujumla utafiti umebaini vijana wengi wenye umri kati ya miaka 13 hadi 17, wana kiwango cha chini  cha stadi za maisha (LifeSkills). 

Alisema matokeo ya mradi huu yanaweza kuwa msingi mkubwa wa kuwafanya Watanzania wawe na maadili na stadi za maisha, kwani ni ukweli kwamba vijana wengi kwa sasa wamekosa stadi za maisha. 

"...Utawakuta vijana wamebweteka wanasema hatuna kazi kutokana na fikra zao za kuamini kazi ni kukaa ofisini tu, kimsingi hizi ni fikra za zamani sana tangu wakati wa Uhuru, hawaamini kwamba zipo kazi zingine zinazoweza kuwasaidia zaidi ya hizo za kukaa ofisini tu,"

"Na hii ni kwasababu wamekosa lile somo la maadili kuliishi licha ya somo la uraia na maadili kufundishwa, labda kuna mahali ambapo halitiliwi mkazo au wanaowafundisha watoto maadili hawajapata ujuzi wa kufundishia wa kutosha. Lakini wazazi turudi nyuma nasi kujiuliza mara mbilimbili, kwamba suala la kutoa elimu si la mwalimu pekee ni suala la jamii nzima yakiwemo makundi yote.

"...Na sisi wazazi tuache kuamini kuwa mtoto anapokwenda shule anakwenda kukariri masomo ili apate 'A' tu kwenye mitihani yake ya mwisho tu, watoto sasa hivi hawajishughulishi, hawajui kazi za mikono zozote hata zile za ndani kama kufanya usafi wake na hata wa nyumba, Wazazi tuache kuamini kuwa alama za juu ndio kipimo cha elimu bora kwa mtoto, sio kigezo pekee cha kwamba mtoto huyu ameelimika."

"...Tunataka kuona mtoto aliye elimika anaweza kutatua matatizo yanayomzunguka iwe ya kijamii, kidini, kisiasa na kiuchumi. Na tuache mihamko, binafsi nimefurahiya sana huu utafiti naombeni mchapishe kwenye vitabu na kusambaza zaidi ili kila mmoja apate," alisema Bw. Lyana.

Aidha aliwataka wazazi kuacha tabia za kuwafungia ndani tu kama glasi, bali kuwafundisha stadi za maisha na maadili ili yaweze kuwasaidia hapo baadaye, "tuache kuamini mtoto akifungiwa shuleni anasoma kuanzia Januari hadi Desemba ndio anapata elimu bora. Tuwaacheni watoto wakae darasani kwa siku 194 na siku zilizosalia tukae nao sisi wenyewe kuwafundisha maadili. 

Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi AliVE Tanzania Bara, Bi. Devocha Mlay akifafanua zaidi matokeo ya utafiti huo uliofanywa ndani ya Wilaya 34 kutoka katika mikoa 18 ya Tanzania na kuratibiwa na Shirika la Milele Zanzibar Foundation, anasema jumla ya vijana 14,645 wenye umri wa miaka 13-17 walifanyiwa upimaji huo kutoka katika kaya 11,802. 

Anasema asilimia 78 ya vijana waliohojiwa walikuwa shuleni na asilimia 22 ni vijana waliokuwa mtaani, wakiwapima katika stadi nne huku ya kwanza ikiwa ni utatuzi wa matatizo. Anasema utafiti umebaini vijana wengi wanauwezo mdogo wa kutambua matatizo na namna bora ya kutatua matatizo hayo. Utafiti umebaini pia vijana wenye elimu ya juu na auelewa wa matumizi wa vifaa vya kidijitali waliweza kutatua matatizo vizuri na mitazamo tofauti ukilinganisha na ambao walikuwa hawana elimu hiyo.

"Umeonesha kuwa asilimia 16.8 ya vijana waliopimwa wanaweza kujitambua wao na wengine, asilimis 53.7 ya vijana waliweza kujitambua wao na kujidhibiti lakini hawakuweza kuwatambua hisia za wengine, huku asilimia 25.5 ya vijana walikuwa hawawezi kujitambua wao wala mitizamo ya watu wengine. "...Kwa mtizamo huu tunaona kuwa vijana wengi wanaweza kujitambua na kujidhibiti lakini hawaangalii kwanini wengine wanafanya vile wanavyofanya, huku katika kupima stadi ya maadili ya heshima kuangalia kijana anavyoweza kujiheshimu, kuheshimu wengine na mazingira. Alisema Bi. Mlay.

ALiVE ipo chini ya Mtandao wa Kikanda wa Elimu na Ujifunzaji (Regional Education Learning Initiatives-RELI), kupitia kongani ya maadili na stadi za maisha (VALi) hii inaratibiwa na Zizi Afrique Foundation NGO iliyoko nchini Kenya, Luigi Giussani Taasisi ya Elimu ya Juu nchini Uganda na Milele Zanzibar Foundation kwa Tanzania. Tathmini ya ALiVE kwa Tanzania bara ilifanywa kwa Ushirikiano wa mashirika mawili; Milele Zanzibar Foundation na Uwezo Tanzania.

No comments:

Post a Comment