WAZIRI DKT DOROTHY GWAJIMA ATEMBELEA BENKI YA NMB - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 25 January 2023

WAZIRI DKT DOROTHY GWAJIMA ATEMBELEA BENKI YA NMB

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna wakati alipowasili Makao makuu ya benki hiyo Januari 24, 2023.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa benki ya NMB Makao makuu alipotembelea benki hiyo Januari 24, 2023.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna akiwa na mgeni wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakifurahia jambo wakati wa kikao na watumishi wa benki hiyo, wakati Waziri Gwajima alipotembelea Makao makuu ya benki hiyo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna (kushoto) akiwa na mgeni wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa kikao na watumishi wa benki hiyo, wakati Waziri Gwajima alipotembelea Makao makuu ya benki hiyo.

BENKI ya NMB imepata nafasi ya kutembelewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum - Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB - Ruth Zaipuna aliembatana na Afisa Mkuu wa Fedha NMB - Juma Kimori, amempokea Mhe. Gwajima na kumuelezea kuhusu masuluhisho yanayogusa moja kwa moja makundi mbalimbali katika jamii.

Lakini pia, aliahidi kushirikiana na serikali  kuhakikisha masuluhisho yao yanakuwa chachu ya maendeleo kwa makundi yote katika jamii kwa kuendelea kuwekeza kwenye teknolojia na ubunifu. 

Katika salamu zake, Mhe. Gwajima alimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wetu pamoja na uongozi mzima wa Benki wa NMB kwa mafanikio waliyoyapata, na kuahidi kuna balozi mzuri kufikisha fursa zinazotolewa na benki hiyo kwa wananchi ili waweze kujijenga kiuchumi.

No comments:

Post a Comment